GAVANA wa Benki kuu ya Tanzania (BOT) Profesa. Frolens Luoga amewashauri wananchi kutumia vyema fedha bila kuziharibu wala kuzichakaza kutokana na ubora na uthamani wa utengenezaji wake.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Prof. Luoga amesema, lazima fedha zitumike kwa uangalifu na kuwaasa wananchi kutumia fedha hizo bila kuzichakaza, kuzitupa wala kuziandika kwa kuwa fedha hizo zinapoharibiwa zinakuwa katika hatari ya kuharibiwa kabisa na mashine maalumu pindi zinapofika benki kuu, na kupelekea gharama ya kupata nyingine kupata fedha hiyo.

Profesa. Luoga amesema kuwa mabenki yana wajibu wa kusaidia benki kuu katika kutekeleza Sera ya Sarafu safi kwa kukusanya pesa zote zilizochafuka na zisizo na hali nzuri na kuzirudisha  benki kuu.

Amesema kuwa fedha ya nchi ina thamani kubwa hivyo lazima matumizi yake yawe ya uangalifu,

"Noti ya Tanzania inatengenezwa kwa gharama zaidi kwani inatengenezwa kwa pamba kwa asilimia 100 ukilinganisha na noti ya dola ambayo hutengenezwa kwa pamba kwa asilimia 75 ya pamba, na hiyo ni kutokana na matumizi" amesema.

Pia amesema kuwa Benki kuu itaendelea kushirikiana na vyombo vya dola katika kuwawajibisha wale wote watakaokutwa na hatia ya kuharibu pesa ambalo ni kosa la jinai.

"Kuchana noti ni kosa la jinai, wengi wamekuwa wakija benki kudanganya ili walipwe tumewabaini walioghushi na waliokamatwa wanachukulia sheria kwa kuwa hiyo sio biashara" Ameeleza Prof. Luoga.

Kuhusiana na malalamiko ya kupungua kwa pesa katika mzunguko Gavana huyo ameeleza kuwa;

" Kila asubuhi tunakutana na kuangaalia hali ya ukwasi katika mabenki na tunajua kila benki ina kiasi gani na tunaweza kutoa mkopo kwa mabenki ili waweze kufanya malipo" ameeleza

Amesema kuwa "Benki kuu inaangalia kiasi cha pesa katika  mabenki yote na kama benki haitakua na pesa tutaangalia ni kwanini na tutasaidia na ikitokea benki haina pesa kwa kutokidhi masharti kama benki tanachukua hatua nyingine" amesema Luoga.

Mwisho amewataka wananchi kutoghushi pesa ya nchi na kwa yeyote atakayekutwa na pesa bandia  atashtakiwa kwa  kosa la jinai na uhujumu uchumi.
 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof Florens Luoga akifafanua alama mbalimbali za zinazopatikana kwenye  Noti ya Tanzania,ambapo alieleza kuwa noti ya Tanzania inatengenezwa kwa gharama,kwani inatengenezwa kwa pamba kwa asilimia 100 ukilinganisha na noti ya dola ambayo hutengenezwa kwa asilimia 75 ya pamba, na hiyo ni kutokana na matumizi" amesema.
  Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof Florens Luoga akionesha moja ya kitabu cha miongozo ya taasisi za fedha mbele ya Waandishi wa Habari wakati wa mkutano huo uliofanyika leo jijini Dar Es Salaam.Kulia ni Naibu Gavana wa BoT,Dkt Bernard Kibesse.Picha na Michuzi JR.
 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof Florens Luoga akisikiliza moja ya swali kutoka kwa mmoja wa Waandishi wa Habari  (hayupo pichani) kwenye ukumbi wa BoT leo jijini Dar es salaam. kulia ni  Meneja Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki (BoT) Zalia Mbeo na katikati ni Naibu Gavana,Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha Dkt. Bernard Kibesse
 Baadhi ya Wanahabari wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo
 Baadhi ya Viongozi waandamizi wakutoka Benki Kuu (BoT),wakifuatilia na kusikiliza mambo mbalimbali yaliyoliyokuwa yakizungumzwa na Gavana wa Benki wa Kuu,Prof Florens Luoga,mbele ya Waandishi wa habari
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof Florens Luoga akifafanua jambo kwa Wanahabari,kushoto ni Naibu Gavana,Utawala na Udhibiti wa Ndani Bw. Julian Banzi Raphael na kulia ni Naibu Gavana,Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha Dkt. Bernard Kibesse

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...