Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe. Ruth Msafiri amewataka wadau wa mazao ya misitu kutambua thamani ya misitu na kuonyesha ushirikiano katika kupambana na matukio ya moto  misituni.

Ameyasema hayo jana Februari 10,2020 wakati alipokuwa akifungua warsha ya siku mbili ya wadau wa misitu  Nyanda za Juu Kusini iliyoandaliwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania  (TFS) iliyofanyika katika ukumbi wa Njombe Mji uliopo katika Mkoani Njombe .

Hata hivyo amewasisitiza wadau kuwa na mipango madhubuti katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na uwepo wa sheria ndogondogo ambazo zitawalazimu wananchi kuzifuata kwaajili ya kuondoa majanga ya moto ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara.

Akimkaribisha Mgeni aliyekuwa Mwenyekiti wa warsha Bw. Bakari Mohamed ambaye ni Afisa Misitu Kutoka TFS amesema kuwa lengo la warsha hii ni kuendelea kukumbushana juu ya kupambana majanga ya moto ya misituni na namna ya ushiriki wa wananchi pindi majanga haya yanapojitokeza.

Bw. Bakari ameongeza kuwa ni vyema  kutambua changamoto zilizopo ili ziweze kutafutiwa ufumbuzi ikiwa ni pamoja na kujua  vyanzo,athari zilizojitokeza na namna ya kukabiliana nazo na jinsi ya kuungana katika kupambana na majanga ya moto.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William amesema kuwa suala la matumizi sahihi ya moto liwekewe mikakati madhubuti ikiwemo ni sambamba na  utoaji wa taarifa za matukio ya moto kwa wakati na sheria zilizowekwa za uanzishaji wa moto kusimamiwa na viongozi wa maeneo husika.

Aidha wadau  wameendelea kuweka msisitizo katika suala la utoaji elimu kwa jamii  lipewe kipaumbele hasa katika  msimu wa kiangazi ambao umekuwa na matukio mengi ya moto.

Warsha hii itaendelea kesho tarehe 11 Februari 2020 ikiwa lengo kuu ni kupanga mikakati endelevu ya udhibiti wa moto wa misituni ambapo mafunzo hayo yamejumuisha wadau kutoka katika taasisi mbalimbali zinazojihusisha na mazao ya misitu Nyada za Juu Kusini.
Pichani: Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe. Ruth Msafiri akizungumza wakati akifungua warsha ya wadau wa misitu ili kujadili mikakati jumuishi ya namna ya kupunguza matukio ya moto Nyanda za Juu kusini yaliyofanyika Mkoani Njombe.
 Pichani: Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe .Jamhuri William akichangia mada wakati wa warsha ya kujadili mikakati jumuishi ya kupunguza matukio ya moto.
 Mwasilisha mada Prof. John Kessy akieleza namna muongozo wa udhibiti wa masuala ya moto unavyotakiwa kufanya kazi na hatimaye kuweka mikakati madhubuti katika maeneo ya vijiji na jamii kwa ujumla
 Picha ya pamoja ya Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe.Ruth Msafiri na baadhi ya  wadau wa misitu kutoka Nyanda za Juu Kusini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...