Charles James, Michuzi TV

WANAWAKE nchini wametakiwa kuacha uoga katika mapambano ya kutafuta fursa za kielimu, uchumi au kisiasa na badala yake wajikite katika kupigania haki yao hasa ya usawa wa jinsia.

Pia wametakiwa kufahamu kwamba hakuna mtu mwingine ambaye atakuja kupigania haki ya mwanamke zaidi ya wanawake wenyewe na wasipofanya hivyo nafasi za kiuongozi watabaki kuzisikia tu.

Hayo yamesemwa na Spika Mstaafu wa Bunge, Mama Anne Makinda jijini Dodoma wakati akizindua kongamano la uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambalo pamoja na mambo mengine limejadili utekelezaji wa maazimio ya ulingo wa Beijing yaliyowekwa miaka 25 iliyopita.

Mama Makinda amesema idadi ya wanawake nchini ni sawa na asilimia 51 ya wananchi wote hivyo kama wataamua kuungana ni rahisi kwao kuweza kutimiza ndoto ya usawa wa kijinsia ambayo kwa miaka mingi imekua ikipiganiwa.

" Tuache uoga wanawake wenzangu, sisi tuna nguvu kubwa sana kwenye jamii zetu, tuna uwezo wa kufanya mambo makubwa na ya kushangaz sana kama tutaamua kuungana kwa pamoja. Niwaase tena acheni uoga.

Hatuwezi kujisifu kwa nafasi zile za upendeleo za viti maalum tunapaswa kuingia ulingoni tushindane na kushinda. Wanawake wengi waliopata nafasi wamefanya makubwa naombeni tujiamini," Amesema Mama Makinda.

Nae Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema hapana shaka kwamba kwa kiasi kikubwa mchango wa viongozi wanawake wastaafu umechangia kwa kiasi kikubwa kuaminika kwa wanawake katika ngazi za kimaamuzi.

" Ni jambo la kujivunia kuwa na wanawake wastaafu ambao wamefanya makubwa na kuifanya jamii iamini kwa wanawake, niwasihi wanawake wenzangu tuamke na kupambana kwa ajili ya haki zetu," Amesema Waziri Ummy.

Kongamano hilo ni la ufunguzi wa siku ya wanawake duniani ambapo kitaifa itafanyika mkoani Simiyu, Kauli mbiu ni 'Kizazi cha usawa kwa maendeleo ya Tanzania ya sasa na baadaye'.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akizungumza kwenye kongamano hilo.
 Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dk Augustino Mahiga akizungumza katika uzinduzi wa kongamano la maadhimisho ya siku ya wanawake lililofanyika jijini Dodoma leo..
 Spika Mstaafu wa Bunge, Anne Makinda (katikati) akizindua kongamano la maadhimisho ya siku ya wanawake. Uzinduzi huo umefanyika jijini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali.
 Spika Mstaafu wa Bunge, Anne Makinda akizungumza wakati wa uzinduzi wa maadhimisho wa siku ya wanawake jijini Dodoma.
 Wananchi na watu mbalimbali wakifuatilia mkutano wa kongamano la maadhimisho ya uzinduzi wa siku ya wanawake ambapo mgeni rasmi alikua Spika Mstaafu Anne Makinda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...