Mkurugenzi wa kampuni ya The look company limited Basilla Mwanukuzi,warembo pamoja na wadhamini wa shindano la Miss Tanzania kwa mwaka huu Grace product pamoja na Amina kwenye picha ya pamoja wakati wa kuzindua shindano hilo jijini Dar es salaam.
   Na Khadija seif, Michuzi Tv
WAREMBO watakiwa kuibeba dhima ya urembo ni heshima na kujua malengo na yao pindi wapewapo taji la  Miss Tanzania ili kusaidia jamii inayowazunguka na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza na waandishi wahabari Mkurugenzi wa kampuni ya The look company limited, Basilla Mwanukuzi amesema kwa mwaka huu wadau wa shindano Hilo watarajie msisimko mkubwa wa aina yake hasa kwa kutumia mfumo mpya wa usahili wa kanda ili kupata washiriki.

" kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kupewa dhamana ya kuendesha shindano la miss Tanzania wadau na wapenda shindano hili wakiwemo na warembo wategemee makubwa zaidi na utofauti wa kipekee kutokana na usahili wa kanda,"

Basilla amefafanua kuwa kamati ya Miss Tanzania itazunguka kanda zote na kufanya usahili,hivyo washiriki kutoka mikoa husika watafanyia usahili kwenye mikoa iliopangwa wa kanda husika.

"Ni mfumo mpya unaotarajiwa kutoa warembo wengi wenye vigezo kujitolea moja kwa moja bila kua na wasiwasi wa gharama za maandalizi ya mashindano lakini kikubwa zaidi ni kuondoa changamoto zilizojitokeza kwa baadhi ya mawakala ambao hawakua waaminifu hasa katika kusimamia warembo,utoaji wa zawadi na usimamizi mzuri wa mashindano kwa ujumla kwa ngazi za mikoa na kanda."

Amebainisha kanda hizo ni pamoja na kanda ya kati ( Dodoma )unaotarajia kufanya usahili machi 7 mwaka huu,kanda ya kaskazini (Arusha) machi 14,kanda ya ziwa(Mwanza) machi 28, kanda ya mashariki (Morogoro) Aprili 4 ,kanda ya vyuo vikuu (Dar es salaam) Aprili 21 ,Kanda ya nyanda za juu kusini (Mbeya) Aprili 11, huku Kanda ya Dar es salaam kwa ujumla kutarajiwa kufanya usahili mei 2 mwaka huu.

Kwa upande wake Miss Tanzania  Mwaka 2019 Sylivia buberwa amesema Mashindano hayo ni nafasi peke ambayo mrembo anaipata katika kutangaza utalii wa nchi yake pamoja na kuisaidia jamii yake kwa namna moja au nyingine kutokana na kuwa balozi pindi apatapo ushindi huo.

 "Taji nilikopewa mwaka jana niliweza kulitumia vizuri na hatimae nimeweza kuiwakilisha vizuri nchi kwenye Mashindano ya Miss dunia na kufanikiwa kuingia ishirini Bora na kuiweka nchi yangu  kwenye historia."

Pia ametoa wito kwa warembo ambao wangependa kushiriki shindano hilo kujitambua,kujiamini pamoja na kuitangaza nchi kwa vivutio vya utalii.

" Kwa mwaka huu tumepata nafasi ya kutangaza vivutio vya utalii hasa misitu yetu nchini kupitia wakala wa misitu (TFS) hivyo ni moja ya nafasi tuliyopewa na kuaminiwa tuifanyie kazi kwa warembo ambao watafanikiwa kuingia kwenye 20  bora ambao watakaa kambi kujiandaa na mchuano."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...