Na Editha Karlo,Kigoma

FAMILIA  ya wasomi wa Chama cha mapinduzi(CCM) mkoani kigoma wanazuoni wametoa tamko juu ya kitendo alichokifanya mbunge wa kigoma mjini mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe cha kupeleka maombi ya zuio la mkopo kwa serikali ya Tanzania bank kuu kwaajili ya kuboresha Elimu.

 Wakizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za Mkoa za chama cha mapinduzi wanazuoni hao wamesema kuwa jambo alilolifanya  Zitto halikubaliki na ni kitendo kisichoungwa mkono kabisa na wanakigoma na hakipaswi kuigwa na mtu yeyote.

"Kitendo alichokifanya Zitto siyo kitendo kizuri kwasababu Zitto ni mbunge kwani ana uwanja mkubwa wa kuzungumza hayo bungeni nasiyo kuandika barua binafsi yeye kama zitto ya kuzuia fedha za mkopo wa kuboresha elimu toka bank kuu"alisema Eliya Michael mwana CCM na mwanazuoni wa Mkoa wa Kigoma

Eliya alisema kuwa Zitto anapaswa kukemewa kwa jambo alilolifanya kukaa kimya watu wataona jambo alilolifanya ni sahihi lakini wao kama wanakigoma wanasema alichokifanya zitto hakipaswi kuigwa na mtu yeyote.

Naye William Mtula mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa alisema kuwa hivi sasa ni wakati wa watanzania kuungana pamoja na kumtia moyo Rais kwa kazi kubwa na nzuri anazozifanya za kuwaletea maendeleo wananchi.

Mtula alisema kuwa matakwa ya Watanzania nikupata huduma bora na za msingi kama vile elimu,afya,miundombinu na zingine.

"Zitto ni mbunge pia ni mwakilishi wa wananchi wa jimbo la Kigoma mjini bungeni hivyo alipaswa kuongelea hoja za wananchi wake na kero zilizopo jimboni kwake na sihayo aliyoyafanya dhidi ya serikali yake"alisema

Wanazuoni hao wamewataka wananchi wa jimbo la Kigoma mjini kulitafakari hilo na kuona sasa ni wakati wao wa kutafuta mwakilishi ambaye atawawakilisha vizuri na siyo yule anayefanya kazi amabazo wananchi hawajamtuma.
 Mwanazuoni na mwanachama wa chama cha mapinduzi(CCM)Eliya Michael akiongea na waandishi wa habari juu ya barua ya Zitto Kabwe kwenda bank kuu kwaajili ya kusitisha mkopo wa elimu kwa serikali
 Baadhi ya wasomi wa chama cha mapinduzi(CCM)wa mkoa wa Kigoma wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya tamko lao kwa mbunge wa kigoma mjini Zitto Kabwe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongereni sana wanazuoni Wa ccm mkoa kigoma kulisemea hili

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...