Waziri wa Maliasili
na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala(kushoto) akibadilishana mawazo na Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kulia) na Watumishi wa Mamlaka ya
Usimamizi wa Wanyapori(TAWA), Wakala wa Huduma za Mistu Tanzania (TFS)
Kanda ya Magharibi na Hifadhi za Taifa(TANAPA) jana mara baada ya ziara
yake ya kikazi Mkoani humo.

Waziri wa Maliasili
na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala, Mkuu wa Mkoa wa Tabora aggrey Mwanri ,
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu na Watendaji wa Mamlaka ya
Usimamizi wa Wanyapori(TAWA), Wakala wa Huduma za Mistu Tanzania (TFS)
Kanda ya Magharibi na Hifadhi za Taifa(TANAPA) wakiwa katika picha ya
pamoja jana kabla hajaanza ziara yake ya siku moja ya kikazi Mkoani
Tabora.


Waziri wa Maliasili
na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala akisamiliana jana na Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Adam Malunkwi wakati alipowasili katika
Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Urambo kwa ajili ya kuanza ziara ya
kutembelea eneo lenye mgogogo katika Maliasili na wakati wa Kata ya
Nsenda.

Mkuu wa Wilaya ya
Urambo Angelina Kwingwa akitoa taarifa ya Wilaya kwa Waziri wa Maliasili
na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala wakati alipowasili kwa ajili ya kuanza
ziara ya kutembelea eneo lenye mgogogo katika Maliasili na wakati wa
Kata ya Nsenda.

Waziri wa Maliasili na
Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala akizungumza na viongozi mbalimbali wa
Wilaya na wale wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo wakati alipowasili kwa
ajili ya kuanza ziara ya kutembelea eneo lenye mgogogo katika Maliasili
na wakati wa Kata ya Nsenda.
Na Mpiga picha wetu
………………………………………………………………………………………………….
NA TIGANYA VINCENT
WATUMISHI wa Mamlaka na Wakala
zilizopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii wametakiwa kuhamia
katika maeneo ya hifadhi ili kulinda na kuzuia uharibifu wa maliasili
kwa ajili ya maendeleo ya Nchi.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa
Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala wakati akizungumza na
viongozi wa Mkoa wa Tabora , Watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa
Wanyapori(TAWA), Wakala wa Huduma za Mistu Tanzania (TFS) Kanda ya
Magharibi na Hifadhi za Taifa(TANAPA) kwenye ziara yake ya kikazi.
Alisema Taasisi zote zinahusika na
usimamizi na ulinzi wa maliasili zinatakiwa kujenga Ofisi ndani ya
Hifadhi na watumishi kuhamia huko ili iwe rahisi kukabiliana na
uharibifu wowote unaotaka kufanyika.
Dkt. Kigwangala aliongeza katika
Ofisi zilizopo nje ya hifadhi wabaki watumishi wachache ikiwemo
Watendaji wakuu na waliobaki waende porini kwa kuwa tayari walishapata
mafunzo ya jinsi ya kupambana na waharibifu wa maliasili.
“Hatuwezi kulinda
maliasili tukiwa maofisini …ni lazima tujenge post kwenye hifadhi zetu
na watumishi wahamie huko wakalinde maliasili zetu , ofisi wabaki
wachache ikiwemo viongozi wa Kanda… wao watakwenda kukagua utendaji kazi
wa watumishi wanaowasimamia” alisisitiza
Alisema ni jukumu lao kuhakikisha
maliasili zilipo ikiwemo wanyamapori , ndege na mimea inalindwa kwa
ajili ya faida ya kizazi cha sasa na kijacho na kuhakikisha wanazuia
uharibifu wowote ndani ya Hifadhi nchini.
Waziri huyo alisema kuwa Kanda ya
Magharibi ndio pekee imebaki na mistu mingi ya asili ni vema watendaji
wanaohusika kulinda na kuhifadhi wakahakikisha haiendelei kuharibiwa.
Katika hatua nyingine Dkt.
Kigwangala ametoa siku 14 kwa Taasisi zilizopo chini Wizara ya Maliasili
na Utalii katika kanda ya Magharibi kukaa pamoja na kuanisha mipaka
halisi ya Hifadhi mpya za Taifa, mapori ya akiba na Hifadhi ya Mistu na
maeneo ya wananchi ili kuondoa mwingiliano na migogoro.
Alisema kumekuwepo na mlingiliano
ambao umetokana na baadhi ya maeneo ya hifadhi moja kusomeka katika eneo
jingine la hifadhi na kuleta utata.
Aidha Dkt. Kigwangala alizitaka
Taasisi hizo kuhakikisha wanaweka upya mipaka katika Msitu wa Hifadhi wa
Ulyankulu ambapo kuna sehemu ambayo wananchi wameshavamia na kufanya
makazi na kujenga huduma mbalimbali.
Alisema mipaka hiyo itasaidia
wananchi kuendelea kuingia katika msitu huo na kuendesha shughuli
mbalimbali ambazo zinatishia uendelevu wa msitu huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...