Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa ofisi yake kilichofanyika Februari 3, 2020 Jijini Dodoma , kushoto kwake ni Mwenyekiti wa baraza hili Bw. Tixon Nzunda ambaye ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo anayeshughulikia masuala ya Waziri Mkuu na Bunge , na kulia ni katibu wa baraza hilo Bw. Paschal Vyagusa.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Waziri Mkuu ambaye ni Katibu Mkuu Bw. Tixon Nzunda akizungumza wakati wa kikao hicho Jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Joachim Zaharani akiwasilisha mada ya Mfumo wa kielekitroniki wa ununuzi wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi la ofisi hiyo lililofanyika tarehe 3 Februari, 2020 Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la ofisi hiyo Bw. Tixon Nzunda kushoto kwake waliokaa, na Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dodoma Bw. Anthelmu Tarimo (kulia kwa waziri) pamoja na katibu wa baraza hilo Bw. Paschal Vyagusa wa kwanza kushoto waliokaa, wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa baraza mara baada ya kikao hicho kufunguliwa rasmi Jijini Dodoma.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Na Mwandishi wetu
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amewaasa watumishi wa Ofisi yake kuendelea kuzingatia sheria na kanuni za utumishi wa umma katika utendaji kazi wao ili kuendelea kuitumikia nchi kwa weledi na ufanisi na kufikia malengo kwa wakati unaostahili.

Ametoa kauli hiyo wakati akifungua kikao cha kwanza cha mwaka cha Baraza la Wafanyakazi la Ofisi hiyo kilichofanyika Februari 3, 2020 Jijini Dodoma.

Waziri Mhagama aliwataka watendaji wote kuona umuhimu wa kuendelea kufanya kazi kwa weledi huku wakizingatia sheria za utumishi wa umma ikiwemo nidhamu kazini, kauli nzuri kwa wateja, kuzingatia mavazi ya staha na kuwahi kazini.

Waziri aliongezea kuwa, ni lazima mtumishi wa umma afanane na kanuni na sheria za kiutimishi kwa kuwa na maadili mazuri awapo kazini na nje ya kazi ili kujipatia sifa njema kuanzia muonekano hadi tabia kwa ujumla.

“Hatutegemei mtumishi wa umma tena wa ofisi hii anakuwa ndiye mlevi wa kupindukia yaani ndiye namba moja Dodoma hii , wala kuvaa mavazi yasiyoendana na hadhi ya utumishi wa umma, hiyo kwetu hatutoivumilia lazima tuikatae na kuhakikisha tunakuwa mfano wa kuingwa,”Alisistiza

Waziri aliwakumbusha watendaji wa ofisi hiyo kuzingatia nafasi zao za kiutendaji wawapo kazini kwa kuzingatia jukumu la ofisi yake ni Kuratibu Shughuli zote za Serikali hivyo lazima iwe ofisi ya mfano.

“Ofisi yetu inaratibu shughuli zote za Serikali , muone ni kwa namna gani sisi ni viungo kwa Serikali hii hivyo mtumie fursa ya baraza hili kukumbushana wajibu wetu kwa kuhakikisha mnatekeleza majukumu kwa nidhamu ya hali ya juu sana,”alisema Waziri Mhagama

Aliutaka uongozi pia kuendelea kuwa na umoja na kufanya kazi kwa kuzingatia dhana ya ushirikishwaji ili kujenga tija kwa kupitia vikao ambavyo vitaibua changamoto zinazowakabili pamoja na kuishauri vyema Serikali kuhusu usimamizi wa kazi na rasilimali watu tunayoisimamia kila siku.

“Ni muhimu kuwa na vikao ili kuendelea kusimamia ustawi sehemu zetu za kazi, na uwepo wa mabaraza haya utaleta tija kwa kuzingatia mchango wake kwa Serikali nzima na hakikisheni mnayatumia kwa kuzingatia dhana ya ushirikishaji,”alieleza Waziri

Aidha aliongezea kuwa ni muhimu viongozi wote kuanzia ngazi ya Vitengo, Idara na Taasisi zote kuendelea kusimamia utekeleaji wa majukumu kwa kufuata sheria, miongozo na kanununi za utumishi wa umma huku wakiwa na upendo kati yao.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Baraza hilo Bw. Tixon Nzunda aliahidi na kumhakikishia Waziri kuwa, watatekeleza maagizo na maelekezo aliyoyatoa ikiwa ni pamoja na kuzingatia maadili mazuri na kuahidi kuendelea kuwajengea uwezo watumishi wa ofisi hiyo juu ya utoaji wa huduma bora inayozingatia viwango vya hali ya juu.

“Tunakushukuru Waziri na nikuhakikishie kuwa unatimu imara, tulivu na chapakazi na tutatekeleza maagizo yote kwa kasi ya mabadiliko ya hali ya juu,”alisema Bw.Tixon

Naye mmoja wa wajumbe wa baraza hilo Bi. Numpe Mwambeja alieleza furaha yake kwa kumshukuru Waziri kwa maelekezo yake yenye nia njema ya kuendelea kuona ofisi yake inakuwa ya mfano katika utendaji kazi wa kila siku na kuahidi kuzingatia maagizo aliyoyatoa.

“Kwa niaba ya wajumbe wenzangu wa kikao cha baraza nimefarijika sana na maagizo yaliyotolewa na waziri ikiwemo kuzingatia suala la uadilifu, kuwahi kazini, kuvaa mavazi ya staha, kuacha uvivu na kuwa na kauli nzuri katika hudumia wateja wa ndani na nje ya ofisi ili kufanya kazi zetu kwa ufanisi unaotakiwa,”alisema, Numpe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...