Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene (kulia)
akisalimiana na Mkazi wa Kijiji cha Chipogoro, jimboni humo, Wilaya ya
Mpwapwa, Mkoani Dodoma, leo, wakati alipokuwa anawasili kwa ajili ya
kufanya ziara, pamoja na kutoa pole kwa wahanga wa mafuriko jimboni
humo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene (kulia)
akimuonyesha Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Jabiri Shekimweri (kushoto),
ardhi ya Kituo cha Polisi Chipogoro, jimboni humo, Wilaya ya Mpwapwa,
Mkoani Dodoma, iliyokumbwa na mafuriko.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene (kushoto)
akimpa pole Mkazi wa Kijiji cha Wiyenzele, Kata ya Chipogoro, jimboni
humo, Wilaya ya Mpwapwa, Mkoani Dodoma, aliyehathirika na mafuriko
yaliyotokea Kijijini hapo hivi karibuni.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene akizungumza
katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji cha Wiyenzele, Kata ya
Chipogoro, jimboni humo, Wilaya ya Mpwapwa, Mkoani Dodoma, leo.
Simbachawene alipkelewa kwa shangwe jimboni humo, wakati alipowasili
baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene (kushoto)
akimpa pole Mtoto wa Kijiji cha Wiyenzele, Kata ya Chipogoro, jimboni
humo, Wilaya ya Mpwapwa, Mkoani Dodoma, ambaye wazazi wake wamehathirika
na mafuriko yaliyotokea Kijijini hapo hivi karibuni.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene (kulia)
akisalimiwa kwa furaha na Wakazi wa Kijiji cha Chipogoro, jimboni humo,
Wilaya ya Mpwapwa, Mkoani Dodoma, leo, wakati alipokuwa anawasili kwa
ajili ya kufanya ziara, pamoja na kutoa pole kwa wahanga wa mafuriko
jimboni humo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene akimuonyesha
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge (wapili kulia) daraja la
Chipogoro lililokumbwa na mafuriko jimboni humo, Wilayani Mpwapwa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
……………………………………………………………………………………………………..
Na Felix Mwagara, MOHA, Dodoma.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene amepokelewa kwa vifijo na nderemo na wananchi wa Jimbo lake baada ya kuteuliwa kuiongoza Wizara hiyo.
Waziri Simbachawene aliwasili jimboni humo saa 4:36 asubuhi, akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ambayo iliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge kwa ajili ya kutembelea maeneo ya Jimbo la Kibakwe Wilayani Mpwapwa ambayo yamekumbwa na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.
Waziri huyo aliwatembelea waathirika wa mafuriko katika makazi yao katika Kijiji cha Wiyenzele na Chipogoro na kuwapa pole kutokana na madhara makubwa waliyoyapata ikiwemo kupoteza nyumba zao, miundombinu, mazao pamoja na mifugo.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji cha Wiyenzele, jimboni humo, leo, Simbachawene alisema amefarijika sana na kuwashukuru kwa mapokezi hayo, na wananchi hao ndio wamefanikisha yeye kuteuliwa na Rais John Magufuli.
“Nashukuru sana kwa kunifanya kuwa Mbunge na Mheshimiwa Rais anazidi kuniamini na amenipa Wizara hii nyeti, inamambo mengi, lakini pongezi zote kwenu kwa kunichagua na pia namshukuru sana Mheshimiwa Rais John Magufuli kwa kunipa nafasi hii,” alisema Simbachawene.
Aliongeza kuwa, Wizara anayoingoza ina taasisi mbalimbali ikiwemo Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji, Idara ya Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), ambazo zinahitaji umakini katika kuziongoza.
Simbachawene pia alitembelea daraja kuu la Chipogoro lililoathiriwa na mafuriko hayo ambayo pia yaliharibu barabara, Kituo cha Polisi, kuchimbua miti, mifugo kusombwa na maji, na watu kujeruhiwa.
“Kituo hiki kwa kweli kimehathiriwa na maji, na kwa hali hii kinapaswa kuhamishwa, mheshimiwa Mkuu wa Mkoa nakubaliana nawe kituo hiki kuhamishwa hapa, na pia tunashukuru kwa kutupatia eneo kwa ajili ya ujenzi wa kituo kipya, nitazungumza na IGP ili tuweze kufanya mchakato wa ujenzi kwa kituo,” alisema Simbachawene.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa huo, Dkt. Mahenge, alitoa pole kwa wananchi hao na huduma mbalimbali zimetolewa na zinaendelea kutolewa kwa wote walioathiriwa na mafuriko hayo pamoja na maeneo ambayo yameharibiwa kutokana na mafuriko.
“Ninatoa milioni tatu hii kwa ajili ya kusaidia wahanga wa mafuriko, na pia timu yetu tangu madhara yatokee ipo hap ana pia Mkuu wa Wilaya kwa pamoja tunafanya kazi ili msipate shida yoyote katika kipindi hiki kigumu,” alisema Dkt. Mahenge.
Pia Dkt. Mahenge aliwataka wananchi wa Kibakwe, wahakikishe wanaendelea kumuweka madarakani kutokana na uwezo wake wa kiutendaji, wasije wakampoteza kiongozi huyo kwasababu kutokana na uwezo wake mpaka Rais Magufuli amemteua kuiongoza Wizara hiyo nyeti.
Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Chipogoro, Hosea Fweda, alisema furaha walizoonyesha kwa Waziri huyo ni kutokana na wananchi kuendelea kuwa na imani naye, kumuhitaji katika kuiongoza Jimbo hilo.
“Uteuzi huu umeonyesha Imani kwake, hivyo kuiongoza Wizara kubwa kama hii, sisi ni furaha yetu, na mheshishiwa Mbunge amekuwa ndani ya siasa kwa muda mrefu, siasa anaijua vizuri, furaha walizoonyesha wananchi wanamaanisha,” alisema Fweda.
Kutokana na mafuriko hayo, wengine waliotoa michango kusaidia wahanga hao ni Waziri Simbachawene, alitoa shilingi milioni moja, Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Jabiri Shekimweri, alitoa shilingi laki tano.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...