Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akihutubia wakati wa Mkutano wa
mashauriano kati ya Serikali na Sekta binafsi ili kusikiliza changamoto
za wawekezaji na wafanyabiashara na kuzipatia ufumbuzi uliofanyika
katika Manispaa ya Shinyanga Februari 26, 2020.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.
Zainab Tellack akieleza kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo katika mkoa
wake wakati wa Mkutano wa mashauriano kati ya Serikali na Sekta binafsi
ili kusikiliza changamoto za wawekezaji na wafanyabiashara na kuzipatia
ufumbuzi uliofanyika katika Manispaa ya Shinyanga Februari 26, 2020.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni akisalimiana na Mhe.Steven Masele (Mb) wakati wa Mkutano huo.

Naibu Waziri Maliasili na Utalii
Mhe. Constantine Kanyasu akijibu hoja wakati Mkutano wa mashauriano kati
ya Serikali na Sekta binafsi ili kusikiliza changamoto za wawekezaji na
wafanyabiashara na kuzipatia ufumbuzi uliofanyika katika Manispaa ya
Shinyanga mkoani Shinyanga.

Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akijibu hoja za masuala ya wafugaji na wavuvi wakati wa mkutano huo.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akijibu hoja za masuala ya
wafugaji na wavuvi wakati wa mkutano huo.

Mmoja wa wachimbaji wadogo mkoa wa
Shinyanga Bw. Ludaki Shaban akiwasilisha kero za ukosefu wa umeme
katika maeneo ya uchimbaji wakati wa mkutano wa kusikiliza changamoto za
wawekezaji na wafanyabiashara katika mkoa huo.

Mmoja wa wafanyabiashara mkoa wa
Shinyanga Bw. Idsam Mapande akiwasilisha hoja zinazohusu kero za
madereva pikipiki wakati wa mkutano huo.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa mkutano huo

Baadhi ya
washiriki wa Mkutano wa mashauriano kati ya Serikali na Sekta binafsi
ili kusikiliza changamoto za wawekezaji na wafanyabiashara na kuzipatia
ufumbuzi uliofanyika katika Manispaa ya Shinyanga wakisikiliza hotuba ya
Waziri wa Nchi Ofisi (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (hayupo pichani)
Februari 26, 2020.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
…………………………………………………………………………………………………….
- MWANDISHI WETU
Zaidi ya
wafanyabiashara na wawekezaji 560 mkoani Shinyanga wamekutana katika
mkutano wa mashauriano baina ya Serikali na Sekta binafsi ili
kusikilizwa na kupata ufumbuzi wa changamoto katika maeneo yao ya
uwekezaji na biashara ili kuendelea kuwa na tija katika maendeleo yao na
nchi kwa ujumla.
Mkutano huo
ulililofanyika tarehe 26 Februari, 2020 ulioandaliwa na Ofisi ya Waziri
Mkuu (Uwekezaji) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkoa wa Shinyanga
na kufanyika katika Ukumbi wa mikutano wa NSSF mkoani humo.
Mkutano
ulijumuisha makundi yote ikiwemo, wakulima, wafugaji, wafanyabiashara
wakubwa na wadogo, wachimba madini, wavuvi pamoja na wenye viwanda na
wawekezaji katika sekta mbalimbali.
Mkutano
ulihudhuriwa na Mawaziri na Manaibu mawaziri kutoka Wizara nane ikiwemo
Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Wizara ya Fedha na Mipango, Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Mambo ya Ndani, Wizara
ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Wizara ya
Maliasili na Utalii na Wizara ya Madini.
Akizungumza
wakati wa kufunga mkutano huo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji nchini Mhe.Angellah Kairuki
alieleza namna Serikali ilivyoendelea na jitihada za kuhakikisha
uboreshwaji wa mazingira ya uwekezaji nchini ikiwa ni pamoja na kutungwa
kwa sheria mpya ya uwezeshaji biashara (Business Facilitation Acts)
Aidha sheria
itasaidia kufanya mapitia ya sera na sheria stahiki kwa lengo la
kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara nchini.
Aliongezea kuwa,
uwepo wa mikutano hiyo inaongeza hamasa kwa wafanyabiashara na
wawekezaji kueleza kero wanazokabiliana nazo pamoja na kupatiwa majibu
ya papo kwa hapo na Mawaziri wa Sekta husika.
“Mikutano
imeibua hoja muhimu zilizopatiwa ufumbuzi na mawaziri wa sekta
mbalimbali niwatoe shaka Serikali itaendelea kuwaunga mkono na ni vyema
mkaendelea kufuata sheria na kanuni zilizopo katika kuwekeza
kwenu,”.alisisitiza Waziri Kairuki.
Naye Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amewahakikishia wafugaji
wa samaki kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira bora ya kuwawezesha
wafugaji kufuga samaki na kueleza kuwa, mabwawa ya samaki yameongezaka
kutokana na jitihada zilizopo na kueleza namna Serikali inavyoendelea
kudhiti uvuvi haramu baharini na maziwa.
Sambamba na hili
Naibu Waziri alieleza kuwa jitihada za ujenzi wa viwanda vikubwa vya
kuchakata mazao yatokanayo na mifugo nchini zinaendelea hivyo wananchi
hawana budi kuwa na matumaini makubwa na Serikali yao.
Aidha Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashantu Kijaji aliwahaikishia wajumbe wa
mkutano huo namna wizara yake ilivyojipanga kuondoa changamoto za
gharama kubwa za mikopo katika benki pamoja na suala la utitiri wa kodi
baada ya kulalamikiwa na wafanyabiashala hao.
“Nimewafurahia
wana Shinyanga kwa uwazi wenu wa kujieleza vizuri, niwahakikishie
kuwa,mwisho wa malalaiko yenu haupo mbali tutahakikisha sekta ya fedha
inatatua kero zenu na kushughulikia upatikanaji wa mikopo na kwa gharama
zinazoeleweka,”alieleza Dkt. Kijaji
Serikali imefanya
jitihada kubwa kuhakikisha Taasisi zetu za mikopo zinashusha gharama za
mikopo (riba) kwa ajili ya shughuli za kijamii zinazowahusu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...