Na Said Mwishehe,Michuzi Blogu ya jamii

KUENDELEA kukithiri kwa athari za mabadiliko ya tabia ya nchi wilayani Ilala jijini Dar es Salaam , asasi mbalimbali za kiraia wilayani humo  zimeungana kwa ajili ya kujenga nguvu ya pamoja kuhakikisha wanakabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia yanchi.

Miongoni mwa nguvu wanayotaka kujenga katika wilaya hiyo ni pamoja na  kuhakikisha kunakuwa wa kutosha kwa jamii kuhusu mabadiliko ya tabianchi ambapo watapata nafasi   na uwezo wa kuripoti changamoto hizo zinapojitokeza.

Mkurugenzi Mkuu wa Asasi ya Kiraia ya FORUM CC, inayoratibu mradi wa mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia ya nchi, unaodhaminiwa na Umoja wa Ulaya (EU), Rebeca Muna, amesema kwamba mradi huo unalenga kujenga mazingira himilivu kuhusu mabadiliko ya tabianchi katika Manispaa hiyo.

Amefafanua kuwa  sababu ya kuhusisha asasi zote wilayani humo, ni kukusanya nguvu na kujengeana uwezo wa kuelimisha jamii kuhusu athari za mabadiliko ya tabia ya nchi na kwa kufanya hivyo itakuwa moja ya hatua muhimu ya kukabiliana na athari za mabadiliko hayo.

"Tunafahamu Wilaya ya  Ilala ni  miongoni mwa maeneo ambayo kimsingi ni kitovu cha Jiji la Dar es Salaam na ndio haswa yaliyoathirika zaidi na mabadiliko ya tabianchi, hivyo ni budi kuanza na mikakato ya kuelimisha jamii, ili kukabiliana na changamoto hiyo.

Amesisitiza kuwa wanataka jmii kuwa na uwezo wa kuripoti,taarifa hizo za mabadiliko ya tabianchi katika maeneo yao na  asasi hizo walizozijengea uwezo na elimu kwa vijana kuhusu  kuchukua fursa kutokana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi kama kubadilisha taka kuwa bidhaa za thamani.

Kwa upande wake Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Makazi (HAFOTA), Kellen Mahimbo, ametumia nafasi hiyo kuelezea kwamba ni muhimu kwa  kila mtu atambue athari za mabadiliko ya tabia ya nchi ili kuweza kukabiliana nazo.

Amesems jamii inapaswa kuwezeshwa kielimu ili iwe na uwezo wa kujenga hoja juu ya athari hizo ili  zimepewa kipaumbele gani na serikali katika kuzikabili.

Wakati huo huo  Jeremiah Wandili ambaye ni  Katibu Mkuu wa Mtandao wa Asasi za Kiraia Kinondoni, amesema msingi wa kukabiliana na athari hizo ni pale wananchi wanapoleta ushahidi wa wazi kuhusu athari hizo kwani wao ndio wanaokutana nazo, na hii itasaidia watunga sera kuchukulia uzito suala hili,” .
 
Kwa kukumbusha tu FORUMCC  kwa muda mrefu imekuwa ikiweka mikakati mbalimbali kupitia miradi iliyojikita kujenga uwezo kwa jamii kutambua namna ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kwa sehemu kubwa wamefanikiwa kuelimisha jamii nini kifanyike kufikia lengo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...