MWENYEKITI wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe Prof.Matthew Luhanga, ameongoza ujumbe wa baraza hilo kukagua maendeleo ya ukarabatina ujenzi wa miundombinu na madarasa kwa ajili ya kuanzisha Shahada za AwaliKampasi ya Dar ss Salaam.

Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Makamu Mkuuwa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka, amesema ukarabati huo na ujenziumekamilika kwa asilimia 98, na kwamba majengo hayo yako tayari kutumika pindiidhini ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania itakapotolewa.

Baraza limepongeza hatua hiyo na kupendekezaujenzi unaoendelea kuendana na mahitaji ya sasa ya mabadiliko ya teknolojia,kwa kuwezesha matumizi ya teknolojia katika ufundishaji.
Muonekano wa baadhi ya majengo yaliyofanyiwa ukarabati na ujenzi.
Meneja Mradi wa ukarabati na ujenzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam-Tegeta, akiwaonesha Wajumbe wa Baraza la chuo hicho maendeleo ya mradi huo.

Wajumbe wa baraza la chuo wakikagua majengo ya Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam-Tegeta.
Wajumbe wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe wakimsikiliza Mwenyekiti wa baraza hilo, Prof.
Matthew Luhanga (wa pili kushoto), wakati walipofanya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam-Tegeta jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe wakiingia katika moja ya majengo wakati walipofanya ziara ya ukaguziwa maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar
es Salaam-Tegeta jijini Dar es Salaam.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka, akifafanua jambo mbele ya wajumbe wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe, walipofanya ziara ya ukaguzi
wa maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar
es Salaam-Tegeta jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe wakimsikiliza Mwenyekiti wa baraza hilo, Prof.
Matthew Luhanga (wa pili kushoto), wakati walipofanya ziara ya ukaguzi
wa maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar
es Salaam-Tegeta jijini Dar es Salaam.


Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Prof. Honest Ngowi (katikati), akizungumza na wajumbe wa baraza la chuo hicho.
Mwakilishi wa Mjumbe wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe, Julius Masota ambaye ni Ofisa Mkuu Msimamizi wa Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango akifafanua jambo wakati wa ziara hiyo.


Picha ya pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...