Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akifungua sherehe za
maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa wafanyakazi wa Benki ya CRDB.
Benki ya CRDB imefanya hafla ya kusherehekea ‘Siku ya Wanawake Dunia’ ikilenga
kuhamasisha usawa wa kijinsia katika jamii. Akizungumza katika hafla hiyo,
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema Benki ya
CRDB inachukulia kwa umuhimu suala la kumuwezesha mwanamke na ndiomana
Benki hiyo imetoa kipaumbele cha ajira kwa wanawake katika ngazi mbalimbali.
“Asilimia 46 ya wafanyakazi wetu ni wanawake, na tunatamani kuona tunaongeza
kufikia asilimia 50,” alisema Nsekela.
Nsekela alisema Benki ya CRDB pia inafanya jitihada za kuwanyanyua wanawake
kupitia nafasi za uongozi huku akibainisha kuwa Benki hiyo ina jumla ya wanawake
viongozi 284 katika ngazi za umeneja, wakuu wa vitengo na wakurugenzi. Nsekela
alisema Benki ya CRDB imedhamiria kujenga mazingira, rahisishi, mazuri na rafiki
ya kujenga usawa ili kuwasidia wanawake waweze kukua katika mazingira yao ya
kazi.
Katika hafla hiyo Benki ya CRDB pia ilizindua kampeni maalum ya kusaidia kutoa
taulo za kike (sanitary pads) kwa wanafunzi mashuleni. Kampeni hiyo ilianza kwa
kuzindua zoezi la uchangiaji lilokuwa likiendeshwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano
wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa ambapo wafanyakazi wa Benki ya CRDB
wamejitokeza kuchangia gharama za ununuzi wa taulo hizo.
“Tunashukuru
Mkurugenzi wetu Mtendaji ametufungulia kwa kuchangia kiasi cha shilingi milioni 1,
hii ni zawadi ya kipekee kwa wanawake wote lakini pia inaonyesha ni kwa namna
gani anawathamini wake,” alisema Mwambapa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Benki ya CRDB, Siophoro
Kishimbo alisema Benki hiyo imeweka mikakati endelevu ya kuhakikisha kuwa
wafanyakazi wanawake wa Benki hiyo wanapata fursa sawa na wanaume.
“Tunaihamasisha jamii kuzingatia usawa katika sehemu zote iwe ni kwenye kazi na
hata nyumbani kwenye familia hii itaongeza ushiriki wa wanawake katika shughuli za
maendeleo na hivyo kujenga taifa imara zaidi,” alisema Kishimbo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akiwatambulisha baadhi ya viongozi wanawake wa Benki hiyo, kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano, Tully Esther Mwamba, Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja, Yolanda Uriyo na Mkuu wa Kitengo cha
Mikikati ya Bishara, Jessica Nyachiro.
Salamu kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, 2020
Mkurugenzi wa Mawasiliano Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akiendesha zoezi la uchangiaji kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa taulo za kike (sanitary pads) kwa wanafunzi mashuleni.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Yolanda Urio akizungumza katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa wafanyakazi wa Benki ya CRDB.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Benki ya CRDB, Siophoro Kishimbo (kulia) akizungumza jambo na baadhi ya waratibu wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa wafanyakazi wa Benki ya CRDB.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wakwanza kushoto), Afisa Mkuu wa Biashara, Dkt. Joseph Witts, Mkurugezi wa Rasilimali Watu, Siophoro Kishimbo na Afisa Mkuu wa Fedha, Fredrick Nshekanabo, wakionyesha vibao vyenye ujumbe wa kuhamasisha
usawa wa kijinsia katika jamii.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakionyesha vibao vyenye ujumbe unaosema “Ninasherehekea Mafanikio ya Mwanamke”.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Benki ya CRDB, Tully Mwambapa na viongozi wengine wanawake wakishangilia baada ya Mkurugenzi Mtendaji, Abdulmajid Nsekela kuchangia shilingi milioni moja kwa ajili ya kusaidia wanafunzi wakike.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...