Mkurugenzi wa Teknohama na Uendeshaji wa benki ya TPB Jema Msuya (kushoto) akikabidhi mifuko 200 ya saruji yenye thamani ya shilingi milioni 3.7 kwa Mbunge wa CCM  Viti Maalum Mkoa wa Rukwa Bupe Mwakang’ata kwa ajili ya kusaidia ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa ya shule mbalimbali Mkoani hapo. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa Reiner Rukalah na Mwenyekiti wa UWT Mkoa Maria Kalula.
 Mbunge wa Viti Maalum wa Rukwa Bupe Mwakang’ata akishukuru baada ya kupokea msaada wa mifuko 200 ya saruji yenye thamani ya shilingi 3.7  kutoka benki ya TPB. Mifuko hiyo itakwenda kusaidia ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa ya shule mbalimbali Mkoani hapo. Kulia ni Mkurugenzi wa Teknohama na Uendeshaji wa benki ya TPB Jema Msuya, na kushoto ni Meneja wa benki ya TPB tawi la Sumbawanga Damas Joseph. Hafla hiyo fupi ya makabidhiano ilifanyika kwenye ofisi za CCM Mkoa wa Rukwa.

  
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa Reiner Rukalah (katikati) akizungumza mara baada ya kupokea msaada wa  mifuko 200 ya saruji yenye thamani ya shilingi milioni 3.7 kutoka kwa benki ya TPB. Mifuko hiyo itakwenda kusaidia ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa ya shule mbalimbali Mkoani hapo. Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum wa Rukwa Bupe Mwakang’ata na kulia ni Meneja wa benki ya TPB tawi la Sumbawanga Damas Joseph. Hafla hiyo fupi ya makabidhiano ilifanyika kwenye ofisi za CCM Mkoa wa Rukwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...