Mechi za Ligi kuu ya soka ya England zitaahirishwa hadi tarehe 3 Aprili kufuatia baadhi ya wachezaji wa ligi hio kupatikana na maambukizi ya virusi vya Corona.
Mashindano yote Ligi ya soka ya Ulaya, mkiwemo Championi Ligi na Ligi ya Ulaya, mechi ambazo zilitarajiwa kuchezwa wiki ijayo, zimeahirishwa kutokana na mlipuko wa coronavirus.
Droo kwa ajili ya raundi ijayo, iliyopangwa kufanyika tarehe 20 Machi, pia imeahirishwa.
Katika Championi Ligi, mechi kati ya Manchester City dhidi ya Real Madrid, Juventus dhidi ya Lyon, Barcelona dhidi ya Napoli na Bayern Munich dhidi ya Chelsea zote zimeahirishwa.
Mechi za Manchester United, Wolves na Rangers katika Ligi ya Ulaya pia zimefutwa.
Mechi zote za robo fainali ya Ligi ya Ulaya ya vijana zilizokuwa zimepangwa kuchezwa tarehe 17 na 18 Machi pia zimesitishwa.
Uefa imesema kuwa maamuzi saidi kuhusu mpangilio wa kuahirisha mechi hizo "yatatolewa baadae".

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...