Charles James, Globu ya Jamii

KATIKA kupambana na maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Corona, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi amegawa vifaa kinga vya kujikinga na ugonjwa huo vipatavyo 3,600.

DC Katambi amegawa vifaa hivyo ambavyo ni vitakasa mikono 'sanitizer' kwa taasisi mbalimbali za umma, binafsi, vyama vya siasa na taasisi za Dini lengo likiwa ni kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huo ndani ya Wilaya yake.

Akizungumza wakati akigawa vifaa hivyo, DC Katambi amesema amechukua hatua ya kugawa ikiwa ni maelekezo aliyotoa ya kuwataka viongozi na wananchi kuchukua hatua za kukabiliana na ugonjwa huo.

Amesema amegawa vifaa hivyo kwa ushirikiano na Mkurugenzi wa Shoppers Plaza ambaye ameeleza kuguswa na namna serikali ilivyochukua hatua ya kupambana na ugonjwa huo ili kulinda wananchi wake.

" Natoa rai na ni ombi langu kwa watu wote ambao wameguswa au kuwiwa kutoa msaada zaidi kusaidiana na serikali yetu katika vita hii kwa kutupatia vifaa tiba au vifaa kinga kwa ajili ya wananchi wangu wa Wilaya ya Dodoma," Amesema DC Katambi.

Amesema vifaa hivyo amevigawa kwa taasisi na maeneo tofauti 23 ambayo ni pamoja na Ofisi za Kata 41 ambazo zimepata vifaa 288, NIDA Wilaya vifaa 144, Vyama vya siasa, vifaa 144, CCM Taifa vifaa 144, CCM Mkoa vifaa 144, CCM Wilaya vifaa 144, Mahakama vifaa 144, Kituo cha Watoto yatima vifaa 144, Vituo vya Wagonjwa wa Wakoma vifaa 144 na Wodi ya akina Mama na Watoto vifaa 144.

Wengine ni Jumuiya ya Wakristo vifaa 144, Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) vifaa 144, Jeshi la Polisi vifaa 144, Jeshi la Magereza vifaa 144, Jeshi la Kujenga Taifa vifaa 144, Wandishi wa habari vifaa 144, pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Wilaya, Vituo vya Afya vya Wilaya hiyo na Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

" Hii ni awamu ya kwanza tunagawa vifaa hivi, bado tutaendelea kushirikiana na wadau wengine katika kufanikisha lengo letu la kupambana na maambukizi ya ugonjwa huu, niwaombe wote kwa pamoja kuungana, kuhamasishana katika kufuata ushauri wa kitabibu unaotolewa na wataalam wetu wa afya.

Nizitake ofisi na taasisi zote ambazo tumezigaia vifaa hivi waweze kuvitumia kama ilivyoelekezwa, hatutomvumilia yeyote ambaye ataenda kinyume na maelekezo ya viongozi wetu wakuu katika vita hii dhidi ya Corona," Amesema DC Katambi.

Kwa upande wake Meneja wa Shoppers Plaza, Ashley Fernandes amesema wameamua kutoa mchango katika mapambano ya ugonjwa wa Corona baada ya kuguswa na jitihada zinazofanywa na Rais Dk John Magufuli katika jitihada zake juu ya ugonjwa huo.

" Kwa kweli tumevutiwa na namna Rais Magufuli anavyopambana kuhakikisha watanzania hawapati madhara makubwa ya Corona, hatua ambazo serikali imezichukua ni kubwa na sisi tumeguswa sana tukaona tutor mchango wetu.

Niwaombe wadau wengine na watu wenye mapenzi na watanzania kuungana kwa pamoja kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huu, kwa kutoa vifaa kinga, elimu au kuhamasisha wananchi kufuata ushauri unaotolewa na wataalam wetu katika kipindi hiki," Amesema Fernandes.
 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi akigawa vifaa tiba ambavyo ni vitakasa mikono kwa muakilishi wa Jeshi la Magereza wa Wilaya hiyo
 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi (kulia) akigawa vifaa kinga kwa muakilishi wa Jiji la Dodoma.
 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi (kulia) akigawa vifaa tiba vya kujikinga na ugonjwa wa Corona kwa muakilishi wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Dodoma.
 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi akizungumza na wandishi wa habari pamoja na viongozi kutoka taasisi mbalimbali waliofika ofisini kwake wakati akigawa vifaa tiba vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

 Meneja wa Shoppers Plaza, Ashley Fernandes ambaye amechangia upatikanaji wa vifaa kinga vya kujikinga na ugonjwa wa Corona akizungumza na wandishi wa habari leo wakati wa kugawa vifaa hivyo.
 Maboksi yenye vitakasa mikono 3,600 ambavyo vinatumika kama mojawapo ya vifaa kinga vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona ambavyo vimetolewa kwa taasisi mbalimbali ndani ya Wilaya ya Dodoma na Mkuu wa Wilaya hiyo, Patrobas Katambi leo.

 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi (kulia) akigawa vifaa kinga kwa muakilishi wa wandishi wa habari waliopo jiji la Dodoma, katikati ni Meneja wa Shoppers Plaza, Ashley Fernandes.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...