Na Shukrani Kawogo, Njombe.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri amewataka wakulima kujiunga kwenye chama cha ushirika ili kuweza kukuza mitaji yao kwa kuitumia Benki ya Maendeleo ya Wakulima (TADB) iliyoanzishwa na serikali kwa lengo la kumwezesha mkulima.
Hayo alitasema katika uzinduzi wa shamba la mfano la upandaji wa miti lenye ukubwa wa hekali mbili uliofanywa na wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) katika kijiji cha Mikongo, Kata ya Kifanya wilayani Njombe ikiwa ni njia ya kuhamasisha jamii kutunza mazingira.
Alisema endapo wananchi watajiunga na banki hii itawawezesha kukuza mitaji yao na kufanya kilimo chenye tija kwani wataweza kulima hekari nyingi zaidi na kupata mazao mengi ambayao yatawaongezea kipato.
Ukiwa mwanachama wa chama cha ushirika utakopesheka kirahisi kupitia benki ya maendeleo ya wakulima pamoja na kupata huduma nyinginezo zenye manufaa kwenu hivyo nawashauri mjiunge ili muweze kunufaika na huduma hizo, Alisema Ruth.
Aidha kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa Umoja wa Wakulima wa Miti Tanzania Kasitoli Timbula amesema kumekuwa na uharibifu mkubwa wa miti hasa katika kipindi cha uandaaji mashamba ambapo miti mingi huungua kwa moto.
Alisema katika kipindi hiki cha uandaaji wa mashamba wakulima huona kazi kufyeka majini yaliyoota shambani mwao na kulazimika kuyachoma moto kitu ambacho hupelekea moto huo kudaka miti na kuiteketeza.
Aliongeza kwa kuwashauri wakulima hao kupanda miti kwa wingi ili na kuacha kufanya uharibifu huo kwani kwa kufanya hivyo ni kutengeneza mazingira ambayo yanaweza kuwasaidia hata vizazi vijavyo.
Hata hivyo kwa upande wa wakulima waliohudhulia uzinduzi huo wamesema elimu hiyo wameipokea kwa mikono miwili hiyo watajitahidi kuwaelimisha na wenzao kuacha kufanya uharibifu wa kuchoma moto na badala yake watunze misitu.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...