Na Said Mwishehe, Michuzi Blogu ya jamii

NAIBU Spika wa Bunge Dk.Tulia Ackson ameamua kutoa maoni yake kwenye mjadala unaoendelea baada ya Rais Dk.John Magufuli kutoa fedha Sh.milioni 38 kwa ajili ya kumsaidia Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa ili atolewe gerezani baada ya kuhumiwa miezi mitano jela au kulipa faini ya Sh.milioni 40.

Amesema kilichofanywa na Rais Magufuli kwa Mchungaji Msigwa ni jambo jema na wakati mwingine watu huwa wanafikiri viongozi hawana ile hisia za kawaida, lakini ukweli unabaki pale pale Rais naye ni  binadamu na anao ndugu zake wengi tu ambao nao wanahitaji msaada wake kama ndugu.

Dk.Tulia amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na Michuzi Blogu ya jamii ambayo ilitaka kupata maoni yake kuhusu hatua iliyofanywa na Rais kwa kutoa fedha hizo ili kumnusuru Msigwa na mijadala inayoendelea hasa mitandaoni ambapo ameeleza kuna watu wanapotosha ukweli kwenye hilo.

"Unaposikia Rais amefanya jambo kama hili kwa ndugu ,tufahamu tu Rais anao ndugu wengi na anawasadia, wengine wanaweza kuwa wamelazwa kwani situnakumbuka jamani, mke wa Rais alikuwa amelazwa na watu walienda kumuona na Rais alikwenda kumuona mkewe.Hivyo watu wajue hata yeye anapitia haya ya ubinadamu, kama binadamu wengine kwani sio malaika,"amesema Dk.Tulia.

Ameongeza pamoja na hayo hilo la kumsaidia  Msigwa, watu wamechukulia wanavyotaka na kila mtu anatafsiri yake na huu ni mwaka wa uchaguzi, hivyo kila mtu anatafuta namna ya kulipotosha ila mwisho wa siku sisi sote kama wanadamu wana ndugu kwenye vyama mbalimbali na haimaanishi mtu akiwa chama kingine basi na udugu unakufa, hapana.

"Hakuna siasa katika jambo hili kwasababu kama angekuwa anafanya siasa na sio hoja ya udugu, basi angefanya kabla ya mahakamani, kwani kesi imekaa muda mrefu na sio kwamba ilianza jana na ikaisha jana, hapana. Rais alikaa mbali wakati kesi iko mahakamani hadi hukumu ilipotolewa.Na ametoa fedha baada ya ndugu zake Msigwa kwenda kutoa ombi kwa Rais Magufuli ambaye naye ana udugu naye,"amefafanua Dk.Tulia.

Hata hivyo amesema kuwa Rais Magufuli amekuwa akisaidia watu wengi na kwa nyakati tofauti lakini kutokana na jambo lenyewe michango yake ilitangazwa hadharani na ndio maana hata yeye alipotoa fedha hizo imetangazwa hadharani na kuongeza kuwa hata CCM nao waliamua kutoa fedha kwa ajili ya mtu wao ambaye ni Dk.Vicent Mashinji.

"Watu wanachangishwa  michango na kwa mazingira hayo lazima watu waambiwe kuwa michango imepungua, CCM walimtoa wa kwao, na huyu(Msigwa) kilichotokea watu wanajaribu kuonesha nani alilipa kwanza na nani alichelewa, sio hoja za msingi na ukiangalia risiti zinavyoonekana chama kilienda baada ya ndugu kulipa na ukisema ndugu sio kwamba Rais ndio alienda pale, hapana, na paleanaonekana kaka yake Msigwa ndio yuko pale na sasa wote wale waliokuwepo pale ni akina Msigwa, hata Gerson naye anaitwa Msigwa,"amesema Dk.Tulia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...