Gavana wa jimbo la Ohio nchini Marekani amesema kuwa ripoti za Idara ya Afya zinaonyesha kuwa, karibu asilimia moja ya wakazi wa jimbo hilo wameambukizwa virusi vya COVID-19 (Corona).

Mike DeWine amesema, anazo ripoti kwamba asilimia moja ya wakazi wa jimbo la Ohio wameambukizwa virusi vya Corona, suala ambalo lina maana kwamba, zaidi ya Wamarekani laki moja wa Ohio wameathiriwa na virusi hivyo.

Mike DeWine ambaye alikuwa akizungumza na televisheni ya CNN ya Marekani amesema yumkini jimbo hilo likafikia kiwango cha kushindwa kufanya vipimo vya Corona kutokana na idadi kubwa ya watu wanaoathiriwa na janga hilo.

Ripoti hiyo imeandamana na ukosoaji mkubwa wa chama cha Democratic dhidi ya serikali ya Rais Donald Trump kwa kushindwa kusimamia ipasavyo mgogoro wa kiafya unaoizonga nchi hiyo.

Daktari Brian Monahan wa Kongresi ya Marekani aliwaambia maseneta wa vyama vya Republican na Democratic kwamba Warekani hadi milioni 150 watapatwa na virusi vya Corona na amewataka viongozi wa nchi hiyo wajiandae kwa hali mbaya zaidi.

Mtandao wa habari wa Truthout nchini Marekani pia umeripoti kuwa Wamarekani milioni 28 hawana huduma ya bima ya afya na kwamba maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo yumkini yakasababisha maafa makubwa. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...