Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka, akihakiki vipimo vilivyotumika katika vyumba vitatu vya madarasa vya shule ya sekondari Chief Kidulile
Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka akihoji sababu ya kufeli wanafunzi wa kidato cha nne katika masomo mengine na kufaulu vizuri kiswahili. Kutoka kulia ni Mkuu wa wilaya Andrea Tsere na kutoka kusho ni mratibu wa elimu kata ya Ludewa Renisi Mtitu na mkuu wa wa shule ya Chief Kidulile Alois Kapelela.


Na Shukrani Kawogo.

Halmashauri ya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe imetakiwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika miradi mbalimbali ya ujenzi inayoendelea wilayani humo ili kujiridhisha na viwango vya ubora vya ujenzi vinavyofanywa na wakandarasi waliokabidhiwa tenda hizo za ujenzi.

Hayo aliyasema Mkuu wa mkoa huo Christopher Ole Sendeka wakati akikagua baadhi ya majengo ya vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya sekondari Chief Kidulile.

Alisema ukaguzi wa mara kwa mara husaidia majengo kuwa na ubora zaidi kwakuwa endapo itaonekana kasoro ni rahisi kuitatua kabla ujenzi haujaendelea kuliko kusubiri ujenzi ukimalizika kitu ambacho kinaleta hatari kwa jingo na kupata hasara.

“ ukaguzi wa namna hii ni mzuri kwani endapo tukisubiri ujenzi ukamilike ndipo tukague hatuwezi kupata viwango sahihi vya ubora matokeo yake badala ya muda zinaanza kuonekana nyufa mbalimbali katika kuta za majengo”, Alisema Ole Sendeka.

Aidha katika hatua nyingine mkuu wa mkoa alihoji sababu ya wanafunzi wa shule hiyo kufeli kwa wingi katika masomo mengine na kufanya vizuri katika somo la Kiswahili ambapo kati ya wanafunzi 113 walifaulu kwa alama za juu wanafunzi 86.

Alimtaka mkuu wa wilaya Andrea Tsere pamoja na mkurugenzi wa halmashauri hiyo Sunday George kukaa kwa pamoja na kumpa tathimini ya shule hiyo huku mkuu wa shule hiyo Bw. Alois Kapelela pamoja na mratibu wa elimu wa kata Bw. Renisi Mtitu wakitakiwa kutoa maelezo ya maandishi juu ya sababu zilizopelekea wanafunzi hao kufeli masomo mengine kwa kiwango kikubwa.

Hata hivyo imeelezwa kuwa moja ya sababu zilizopelekea wanafunzi hao kufaulu somo hilo la Kiswahili kwa kiwango hicho ni kutokana na mwalimu huyo kujitolea muda wa ziada kuwafundisha wanafunzi hao na kuhakikisha kuwa wanalielewa vizuri somo hilo.

“ Kama mwalimu huyu ameweza kujitolea muda wake wa ziada kufundisha mpaka watoto wamefanya vizuri nyie walimu wa masomo mengine mmeshindwaje kujitolea ili wanafunzi wafaulu vizuri? Kama wanafunzi wameweza kumuelewa mwalimu wa Kiswahili nyie mmeshindwaje kufundisha mkaeleweka kama mwenzenu?”, alihoji Ole Sendeka.

Aidha Ole Sendeka alifurahishwa na juhudi hizo za mwalimu huyo aliyefahamika kwa jina la Hnipha Mbambano ambapo alimzawadi dola 100 ambayo thamani yake kwa pesa ya kitanzania ni sawa na laki mbili na thelathini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...