Mkami Zakaria (30)mtuhumiwa wa mauaji ya binti wa kazi eneo la Elkuirei wilayani Arumeru akiingizwa mahakamani chini ya Askari kanzu wa kike kwenye mahakama ya hakimu mfawidhi wilaya hiyo leo Gari iliyombeba mtuhumiwa wa mauaji ikitoka nje ya mahakama ya hakimu mfawidhi wilaya ya Arumeru picha zote na



Na Vero Ignatus Arusha


Taharuki imetanda kwenye mahakama ya hakimu mkazi Arumeru wakati mtuhumiwa wa mauaji ya binti wa kazi Mkami Shirima baada ya kufikishwa chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi wenye silaha kali na mabomu ya machozi.

Katika hali ya kushangaza Polisi waliokuwa wamemleta mtuhumiwa Mkami Shirima (30) wa kesi namba 5 /2020 ya kumuua Msichana wa kazi Salome Zakaria( 18) wamewazuia waandishi wa habari kusikiliza kesi ya mtuhumiwa huyo kwenye Mahakama ya Wilaya ya Arumeru iliyopo Sekei Mkoani Arusha.

Mtuhumiwa huyo aliyeletwa mahakamani leo majira ya saa 4 asubuhi akiwa na gari namba T920 AUB aina ya Nadia kisha kukaa kwa muda na kupandishwa mahakama ambapo kabla ya kufikishwa mahakamani yaliandaliwa mazingira na polisi waliokuwa eneo hilo kwa kuanza kuwapanga wanahabari jinsi ya kupiga picha na kisha kuwafukuza wananchi waliofika mahakamani hapo kwa kuamuru watoke nje ya geti la mahakama

Baada ya wananchi kutoka nje ya geti polisi hao waliweka ulinzi kisha kumshusha mtuhumiwa Mkami kwenye gari na kumwongoza kuingia mahakamani huku wakizuia wanahabari kuendelea na majukumu yao kwa kigezo cha mahakama kuwa na chumba kidogo cha kusikiliza


Wakati wanahabari wakiwa na kibali mkononi polisi hao waliweka vizingiti kuwa chumba cha mahakama ni kidogo hivyo hata wanahabari hawawezi kuingia huku hata wao wakijisahau kuwa ni wengi kuliko wanahabari

Awali akisomewa shtaka lake la mauaji jana Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Arumeru,Amalia Mushi alisema Mkami mkazi wa mianzini mnamo Machi 6/2020 alimuua Salome Zakaria

Na kuahirisha kesi hiyo hadi Machi 26 mwaka huu itajapokuja tena kutajwa tena huku mtuhumiwa akipelekwa mahabusu Gereza la Kisongo

Baada ya kusomewa mshtakiwa alitolewa tena kwa mbwembwe za polisi akitumia gari nambaT497 DEM aina ya Raumu huku akiongoza na difenda moja mbele ya polisi na difenda nyingine nyuma

Pia wananchi waliohudhuria kesi hiyo walikuwa na jabza na kuhoji ni kwanini wamezuia wananchi kuingia mahakamani kufuatilia kesi hiyo?

Jambo hilo limeibua sintofahamu ambayo inaonyesha Polisi hao kumlinda mtuhumiwa ambaye ni mke wa Askari Mwenzao na kuleta hisia tofauti kwa waandishi wa habari kuzungushwa kupata kibali Cha kuandika habari hiyo.

Awali kwa mujibu wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha mtuhumiwa alianza kumpiga marehemu Machi 5 mwaka huu nyumbani kwake Maeneo ya mianzini ambapo baada ya kufanya tukio hilo, mtuhumiwa alimfungia ndani kwake hadi ambapo hali ya merehemu ilibadilika na kupelekwa hospitalini kwaajili ya kupatiwa matibabu.

Marehemu alifariki siku ya 9/3/2020 muda wa saa 8:00 asubuhi wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Maunt Meru baada ya kupigwa na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake na mtuhumiwa huyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...