Na Amiri kilagalila,Njombe
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe mkoani humo Ally Juma Ally ameihakikishia kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za serikali za mitaa LAAC kuwa halmashauri hiyo inategemea kuanza kutoa huduma za afya katika hospitali mpya ya wilaya mapema itakapofika mwezi wa saba mwaka huu.

Bwana Ally Juma ameieleza kamati kuwa majengo ya hospitali ya halmashauri ya wilaya yamekamilika kwa zaidi ya asilimia 98,hivyo hakuna jambo lolote litakalo kwamisha kuanza kutoa huduma kwa kuwa shughuli ndogo zilizobakia zinaendelea kushughulikiwa.

“Kama mnavyoona majengo haya yamekamilika kazi iliyobaki ni kazi ya kuweka mifumo,kuchimbo mashimo ya taka,lakini tumeshafunga milango,vioo vipo tayari na tumeshavuta umeme kutoka barabarani kwa hiyo hatua tulizofikia ni kama asilimia 98 au 99 na tumebakiwa na shughuli ndogo ndogo ambazo piga ua lazima julai tuanze kutoa huduma hapa”alisema Ally Juma Ally

Aidha Mkurugenzi amesema mradi wa ujenzi wa hospitali  ya wilaya ya Njombe,mpaka sasa umetumia bilioni 1.5 iliyotolewa na Rais Magufuli lakini halmashauri hiyo ilitenga milioni 100 kwa ajili ya kuchangia mradi huo na mpaka sasa imekwishatoa milioni 65.

Hata hivyo bwana Ally Juma ametaja sababu za kuchelewa kukamilika kwa mradi huo ni pamoja na mvua kubwa zinazonyesha katika wilaya ya Njombe.

“Huu mradi tungemaliza mapema sana lakini changamoto kubwa iliyotusibu ni mvua,kwa hiyo masika ilibidi tusimamishe ujenzi,lakini changamoto nyingine ya pili tulikuwa tunasafirisha material umbali mrefu sana,lakini tunajito kupambana ili majengo haya yaweze kukamilika”alisema tena Ally Juma

Edward Mwalongo ni mbunge wa jimbo la Njombe mjini na Ezekiel Maige ni mbunge wa jimbo la Msalala ambao ni miongoni mwa wajumbe wa kamati ya LAAC walihoji vigezo vilivyotumika kujenga hospitali hiyo ya wilaya katika kata ya Matebwe ambayo ipo takribani kata za mwisho za wilaya,ambapo mkurugenzi amekiri kujengwa katika maeneo hayo kutokana na sababu mbali mbali

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa kamati LAAC Abdalah Chikota amepongeza kasi ya ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo na kuomba sasa huduma inaanza kutolewa katika majengo hayo.

“Mkurugenzi na DMO sasa hakikisheni tunakwenda kwenye matumizi ya hii hospitali na sisi lengo tuone huduma imeanza kutolewa,kwa majengo mmejitahidi kusimamia na hali inaonekana sasa nguvu kubwa tuelekeze kwenye matumizi ya haya majengo”alisema Chikota.

Hospitali ya wilaya ya Njombe ni miongoni mwa hospitali 67 zinazojengwa hapa nchini kwa ghalama ya shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na Rais kwa wilaya tofauti tofauti huku ikitakiwa kujengwa majengo 7 kwa kutumia mafundi wa ndani.

Aidha kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za serikali za mitaa ikiwa wilayani Njombe,wabunge wamefanikiwa kukagua mradi huo wa ujenzi wa hospitali inayojengwa kata ya Matembwe,Mradi wa maji wa Kidegembye pamoja na mradi wa umwagiliaji wa kikundi cha Twilumba uliopo kijiji cha Itipinga kata ya Igongolo na kuridhishwa na miradi hiyo.
Mkurugenzi wa halmashauri ya  wilaya ya Njombe bwn Ally Juma Ally akiieleza kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za serikali ulipofikia mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Njombe


Baadhi ya majengo ya hospitali ya wilaya ya Njombe wakati yakikaguliwa na kamati ya bunge ya kuduma ya hesabu za serikali za mitaa.
 Makamu mwenyekiti wa kamati ya LAAC akizungumza mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Njombe
 Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri akinawa mikono kutokana na tahadhari ya korona mara baada ya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Njombe.
Kamati ya bunge ya kudumu ya hesabu za serikali za mitaa wakizungumza katika mradi wa umwagiliaji uliopo Kijiji cha Itipingi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...