Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amesema Jeshi la Polisi limejipanga vizuri katika kuhakikisha linakabiliana vyema na matukio ya uhalifu yanayojitokeza nchini na kwamba Jeshi lipo imara hasa kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.
IGP Sirro amesema hayo wakati akikamilisha ziara yake ya ukaguzi katika Kanda Maalum ya Polisi Jijini Dar es salaam kwa kutembelea Makao Makuu ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia, ambapo amewataka askari wa vyeo mbalimbali kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kufuata sheria.
Kuhusu Corona, IGP Sirro amesema kuwa, Jeshi la Polisi limechukua hatua madhubuti ikiwemo kutoa elimu kwa askari wa vyeo mbalimbali na wateja wanaofika kupata huduma katika vituo vya Polisi kuhusu kujikinga ili kuendelea kudhibiti kusambaa kwa maambukizi ya ugonjwa wa corona.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...