Na Said Mwishehe,Michuzi Globu ya jamii

 WATU Watano ambao ni maarufu kwa ukataji watu mapanga maeneo ya Tegeta jijini Dar es Salaam wanashikiliwa na Jeshi la Polisi baada ya kukamatwa kutokana na uporaji walioufanya katika nyumba ya Ofisa wa Serikali Victor Nelson  Nyirenda ambaye kabla ya kumpora walimkata mapanga kichwani.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amewataja watuhumiwa hao leo Machi 27,2020 kuwa ni Juma John( 27), Japhet Charles( 25), Victor  William ( 23), Joseph Charles (28) na Anthony  Christian( 40) na kwamba walivamia nyumba ya Ofisa huyo Januari 22 mwaka 2020 saa 7:30 usiku.

Amefafanua watu hao waliingia kwenye nyumba ya Ofisa huyo maeneo ya Tegeta jijini Dar es Salaam na kumjeruhi kwa kumkata mapanga na kisha  kufanya uporaji wa simu aina ya Samsung mbili, Laptop HP, pochi na bahasha iliyokuwa na shilingi 500,000 na kufanya uporaji wa vitu kuwa na thamani ya jumla Sh.3,765,000.

'Baada ya uhalifu huo Jeshi la Polisi kupitia kikosi maalum kilianza kufuatilia na kufanikiwa kuwakamata watu wote waliohusika kufanya uporoaji huo nyumbani kwa Victor Nyirenda. Na upelelezi wa tukio hilo uliendelea na Machi 16 mwaka huu tulifanikiwa kuwakamata wahalifu wengine wanne ambao wamekuwa wakipokea vitu vya wizi kutoka kwa watu hao na kisha kuviuza,"amesema.

Kamanda Mambosasa ameongeza kuwa baada ya kufanya upekuzi kwa watu hao kwenye maeneo ambayo wamekuwa wakiuza vitu hivyo vya wizi walifanikiwa kupata laptop 34, simu 10, luninga, deki na chaji za laptop. Watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani kwa ajili ya kujibu tuhuma zinazowakabili .

Wakati huo huo Kamanda Mambosasa amesema pia  jeshi hilo limefanikiwa  kukamata silaha mbili ikiwemo ya Short Gan  yenye namba 011822114 Mali ya OK Security iliyopotea katika Kanisa la EAGT City Centre Mtoni Mtongani jijini Dar es Salaam mali ya Kampuni ya Ok Security.

Mambosasa amesema Machi 26 mwaka huu saa 10 jioni katika eneo la Kanisa iliyopatikana silaha hiyo iliyokuwa imepotea katika mazingira ya kutatanisha na kwamba kwa sasa walinzi wawili wanashikiliwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi kutokana na mazingira ya kupotea na kupatikana kwa silaha hiyo.

Aidha amesema jeshi hilo  limefanikiwa kupatikana kwa  silaha aina ya Maker Four iliyokuwa imetelekezwa katika ghala la ENKA Enterprises Company na risasi  72 na kwamba Polisi wanaendelea na uchunguzi wa kubaini mmiliki  wa silaha hiyo na kubaini kama imeshawahi kutumika katika matukio ya uhalifu.
 Baadhi la Kompyuta Mpakato zilizo kamatwa na Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam.
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa akionesha mabegi ambayo majambazi walitumia kuweka Kompyuta mpakato na kuzifikisha kwa wahifadhi kompyuta hizo.
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa  akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, baada ya kukamata vitu mbaimbali zikiwepo Ccompyuta mpakato na bunduki.
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa akionyesha baadhi ya maboksi ya Compyuta mpakato zilizokamatwa na Jeshi hilo zinazotumika kuwekea Kompyuta hizo wanapotaka kuziuza
 Baadhi ya Risasi zilizokamatwa na jeshi la polisi kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa  akionesha Bunduki zilizokamatwa na Jeshi hilo pamoja na risasi 72 ambazo zilikamatwa.
 Baadhi ya Kompyuta mpakato na luninga zilizokamatwa na jeshi la polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...