Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa 11 kwa kosa la wizi kwa njia ya mtandao. Watuhumiwa hao walikuwa wakitumia majina ya watu katika akaunti zao kwa njia ya kujipatia fedha.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya   Ulrich Matei amesema kuwa watuhumiwa walikuwa wanajihusisha na  wizi kwa kutumia majina ya viongozi na wasanii kwa kusambaza ujumbe wa kuomba fedha kwa watu wengine wenye mahusiano ya viongozi na wasanii.

Wanaoshikiliwa na Jeshi hilo kwa tuhuma ya wizi kwa njia ya mtandao ni  Alfred Kigunga (22) Mkazi wa Mtaa wa ZZK-Mbalizi, George Mathias Bembeja (24) Mkazi wa Mtaa wa  Kanama-Mbalizi ,Eliud Emili Mahenge (24)Fundi Rangi, Mkazi wa mtaa wa Kanama - Mbalizi, Philipo Emanuel Yawalanga   (22)Mkazi wa  Mtaa wa Ndola-Mbalizi, Gasto Goodluck Sanga (21) Mkazi wa mMtaa wa Tunduma Road-Mbalizi, John Michael (21) JOHN MICHAEL [21] Mkazi wa ZZK-Mbalizi,Emmanuel Edwine (28) Kalelo Mkazi wa Tunduma Road,Daud  Exavery Sanga (23) Mkazi wa ZZK-Mbalizi, Junior  Ally Kawanga (21) Mkazi wa Songea Mkoani Ruvuma,Kasto Nebar Tweve (22) Mkazi wa Chapakazi Mbalizi pamoja na Alpha Kayoka (23)Mkazi wa Tarafani Mbalizi.

Watuhumiwa walikamatwa kati ya Februari 21 na 22 mwaka huu baada ya Jeshi la Polisi Mkoani hapa kufanya msako katika maeneo ya Mji mdogo wa Mbalizi Jijini Mbeya na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa kumi na moja (11) wanajihusisha na wizi kwa njia ya mtandao kwa kutumia akaunti batili za mtandao wa Facebook zenye baadhi ya majina ya viongozi wa Serikali na wasanii maarufu wa hapa nchini.

Kamanda Matei amesema kuwa watuhuhumiwa hao  wanafanya uhalifu  kwa  kufungua akaunti za “facebook” zenye majina ya baadhi ya viongozi wa serikali na wasanii maarufu na kuuaminisha umma kwa kuweka picha za viongozi na wasanii hao na taarifa zingine kwenye akaunti hizo kisha kuzitumia akaunti hizo kutangaza Utoaji wa mikopo nafuu,Nafasi za Kazi/Ajira ,Nafasi Fursa ya kuendeleza vijana wenye vipaji vya usanii na kuwataka wananchi ambao wapo tayari kutumia fursa hizo kutuma fedha kati ya shilingi 20,000 ihadi Sh.30,000 ikiwa ni bima kwa wanaohitaji mikopo nafuu au gharama ya fomu kwa wanaohitaji ajira.

Aidha  wahalifu hao huweka namba za simu kwa ajili ya wananchi kutuma fedha ambapo namba hizo kununua kwa mawakala wa kusajili laini wasiowaaminifu ambao hutumia namba za NIDA za wateja kusajili laini bila wateja hao kujua na laini hizo kuwauzia wahalifu kati ya shs.1,000 mpaka sh.5,000.

Watuhumiwa wamehojiwa na kukiri kufungua akaunti mbalimbali batili za “facebook” za Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani  Joketi Mogelo na akaunti 13 za wasanii maarufu ambao ni Wema Sepetu, Aunt Ezekiel,Jacqueline Wolper na Kajala  Masanja.

Kamanda Matei amesema  kati ya watuhumiwa kumi na moja (11) wawili ni Mawakala wa kusajili laini kwa kutumia vitambulisho vya NIDA ambao wamekiri kuuza laini hizo kwa wahalifu ambazo wamezisajili kinyume na utaratibu kwa kutumia namba za NIDA za wateja bila wateja hao kufahamu.

Kamanda Matei ametoa wito kwa mwananchi yeyote ambaye amewahi kutuma fedha kwa wahalifu kupitia akaunti hizo batili kufika Makao Makuu ya Polisi Kitengo cha Upelelezi wa Makosa kwa njia ya mtandao.

Matei amewaasa wananchi kuwa makini wanapokwenda kusajili laini zao, wasiruhusu namba za vitambulisho vyao vya NIDA kutumika kusajilia laini za watu wengine pamoja na namna ya kuangalia namba za simu zilizosajiliwa kwa namba za NIDA kama ilivyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ni *106# itakupa maelekezo ambayo utachagua option namba mbili  ambayo itakupa maelekezo uingize namba ya kitambulisho chako cha NIDA, badae itakupa orodha ya namba za simu zilizosajiliwa kwa kutumia namba ya kitambulisho hicho.

Hata hivyo amewataka wananchi kuwa makini na taarifa zinazotolewa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ambazo zinaelezea fursa mbalimbali, masomo, biashara na mikopo ambazo zinawataka kutuma kiasi kadhaa cha fedha ikiwa ni moja ya masharti ya kupata fursa hizo, ni vyema kujiridhisha kwenda mamlaka za serikali zilizo karibu kwa ajili ya kujiridhisha kabla ya kufikia hatua ya kutuma fedha.

Mashauri yao yanaendelea yakishakamilika watawafikisha mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...