Na Cathbert Kajuna, Globu ya Jamii.
Kamati
ya Bunge ya kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira imewapongeza
Wakala wa Vipimo (WMA)kwa kufanya kazi kisasa ili kuendana na sera ya
Serikali kuelekea Uchumi wa Viwanda.
Akizungumza
na wanahabari mara baada ya ziara ya kutembelea kituo hicho Mwenyekiti
wa kamati ya Bunge ya kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe.
Suleiman Ahmed Saddiq amewataka kuendelea kujituma kwa kufata sheria na
taratibu za upimaji.
“Kiukweli
nimefurahi kufika mahali hapa na kujionea mambo mengi yanayofanywa
kisasa na wakala wa Vipimo katika kituo cha Misugusugu Kibaha - Pwani
hivyo niwaombe waendelee kuchapa kazi kwa bidii," amesema Mhe. Saddiq.
Ameongeza
kuwa Wakala wa Vipimo wamekuwa msaada mkubwa katika kutatua changamoto
hasa katika upimaji magari na upimaji wa mita za maji na kuziomba
mamlaka za maji ikiwemo DAWASA,DUWASA, MURUWASA lazima zote zipitie hapa
WMA na kuhakikiwa kisha kupewa kibari tayari kutumika kwenye jamii.
Kwa
upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa wakala wa Vipimo (WMA), Ludovick
Manege, amesema mafanikio ya kituo hicho yametokana na kujituma na
kupata ushirikiano mkubwa kutoka Serikalini kwa kutatua baadhi ya
changamoto.
Amesema
mpaka sasa kituo hicho kimepata mafanikio makubwa kwa kuendelea
kusimamia misingi na kanuni bora katika upimaji wa matenki ya mafuta na
dira za maji.
"Tumepewa dhamana ya kuhakikisha matenki ya mafuta yana hakikiwa hapa,
yanapoenda kujazwa mafuta, na Dira za Maji zinazoletwa nchini zote
lazima zipimwe ili kuhakikisha mamlaka za maji zinatumia mita sahihi”
amesema Ludovick.
Mjumbe wa kamati ya bunge viwanda, biashara na mazingira akiuliza swali mara baada ya mara baada ya katika kituo Wakala wa Vipimo kilichopo Misugusugu kilichoko mkoani Kibaha - Pwani.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge Viwanda, Biashara na Mazingira mheshimiwa Suleman Saddiq mbunge wa Mvomero (aliyenyoosha mikono) akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Vipimo Kituo cha Misugusugu Kibaha - Pwani, Alban Kihuld (wa tatu toka kushoto).
Wabunge wa kamati ya kudumu ya bunge Viwanda, Biashara na Mazingira akitembelea katika kituo cha Wakala wa Vipimo kilichopo Misugusugu Kibaha- Pwani.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge Viwanda, Biashara na Mazingira mheshimiwa Suleman Saddiq mbunge wa Mvomero akieleza jambo kwa vyombo vya habari mara baada ya kupata maelezo juu ya utendaji kazi na majukumu ya Wakala wa Vipimo mara baada ya katika kituo cha Misugusugu kilichoko mkoani Kibaha - Pwani.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo Dkt. Ludovick Manege akiongea na wanahabari juu ya huduma zinazotolewa na wakala wa vipimo mara baada ya kutembelewa na wabunge kamati ya bunge viwanda, biashara na mazingira katika kituo chao cha Misugusugu kilichoko mkoani Kibaha - Pwani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...