Na Mwandishi Wetu Arusha
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imeitaka Serikali kuongeza na kutoa fedha za miradi ya maendeleo ya jamii katika Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru na Vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini.
Akitoa maelekezo kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inayosimamia Taasisi ya Maendeleo ya Jamii leo tarehe 16/03/2020 mkoani Arusha Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Peter Serukamba ametaka bajeti ya maendeleo ipelekwe katika Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru na vyuo vya Maendeleo ya Jamii ili kuweza kutekeleza miradi ya maendeleo.
Ameongeza kuwa kada ya Maendeleo ya Jamii ni muhimu kwa maendeleo ya jamii hivyo, nguvu kubwa inahitajika katika kuwekeza kwenye Taasisi na Vyuo vya Maendeleo ya Jamii ili kupata wataalam wa Maendeleo ya Jamii watakaoleta mabadiliko katika taifa.
" Hili ni suala gumu kwa Taasisi na Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kujitoa na kufanya kazi bila bajeti ya maendeleo, wapeni Bajeti wafanye makubwa" alisema
Amesisitiza uongozi wa Wizara Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii kusimamia Taasisi na Vyuo vya Maendeleo ya Jamii chini ya Wizara ili viweze kuwa na tija kwa maendeleo ya taifa kwa kuzalisha wataalam watakaosidia kuleta mabadiliko katika jamii.
Akitoa taarifa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru imefanya ukarabati na ujenzi wa majengo mbalimbali ikiwemo Maktaba ya kisasa yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 1008 kwa wakati mmoja.
Ameongeza kuwa Taasisi imejipanga katika kutatua changamoto zilizopo ikiwemo kutenga fedha za ndani zitakazosaidia kutatua changamoto za miundombinu na utawala.
"Tumekuwa na changamoto nyingi za miundombinu katika Taasisi yetu na tumejipanga kwa kutenga fedha za ndani ili kusaidia kuondokana na changamoto zinazotukabili" alisema.
Amesema kuwa Taasisi imeanzisha vituo muhimu katika maendeleo ya nchi ikiwemo Kituo cha kidijitali chenye lengo la kuandaa mawazo na kuzalisha miradi mbalimbali kwa wanafunzi na wananchi ili kuwawezesha kiuchumi na kituo cha machapisho ya wanawake kinacholenga kutoa fursa mbalimbali za kiuchumi hasa kwa wanawake.
Mmoja wa wanufaika wa Kituo cha kidijitali cha Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru kutoka Kitomary HotCulture Project Bw. Joshua Kitomary amesema kituo hicho kimemsaidia kuanzisha biashara, kulima maharage mabichi na ameweza kuajiri wafanyakazi wa kudumu kumi na wafanyakazi wa muda100.
"Kituo cha Kidijitali kimeniwezesha na pia nilijidunduliza katika mkopo nilioupata wa masomo na kuwekeza katika kilimo. Niliwekeza shillingi Milioni moja na inanipa faida ya shilingi Milioni mbili na laki sita" alisema
Akichangia katika majadiliano ya Taarifa ya Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Mjumbe wa Kamati hiyo, Hawa Ghasia ameishauri Taasisi kuzidi kuwekeza zaidi katika Taasisi iliyopo Tengeru kuliko kuwaza kuanzisha matawi ya Taasisi hiyo katika mikoa mingine.
"Niwapongeza kwa kuzingatia masuala ya kijinsia katika utendaji kazi wa Taasisi ambapo wanawake wamepewa nafasi sawa na wanaume katika utekelezaji wa majukumu ya Taasisi, wekezeni hapa Tengeru ndio historia ilipo" alisema
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imetembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru iliyopo chini ya Wizara Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Peter Serukamba (kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu (kulia) wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ilipotembelea Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru kukagua miradi ya maendeleo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Peter Serukamba (kulia)akitoa maelekezo kwa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara kukagua miradi ya Maendeleo katika Taasisi hiyo kushoto ni Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu.
Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akitoa taarifa ya utekelezaji miradi ya maendeleo ya Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara kukagua miradi ya Maendeleo katika Taasisi hiyo kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Peter Serukamba.
Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Dkt. Bakari George akitoa ufafanuzi kwa masuala mbalimbali kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara kukagua miradi ya Maendeleo katika Taasisi hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Peter Serukamba (kushoto) na Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu wa tatu kushoto pamoja na wajumbe wa Kamati wakikagua miradi ya Maendeleo katika Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru wa pili kushoto ni Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Dkt. Bakari George na wapili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya uendeshaji Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Dkt.Lilian Mwaipopo .
Mkutubi Mkuu wa Maktaba ya Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Bw. Joseph Suluma akitoa maelezo kuhusu maktaba hiyo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara kukagua miradi ya Maendeleo katika Taasisi hiyo.
Mratibu wa Kituo cha Kidigitali Jamii Outreach cha Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Evelyn Rwela akitoa maelezo kuhusu kituo hicho kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara kukagua miradi ya Maendeleo katika Taasisi hiyo.
Mratibu Kituo cha Tafiti na Machapisho kilichopo katika Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru kuhusu Wanawake Bw. Ebenezer Lau akitoa maelezo kuhusu kituo hicho kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara kukagua miradi ya Maendeleo katika Taasisi hiyo.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...