Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso, akijaribu ubora wa mataruma yanayotengenezwa katika Kiwanda cha Mataruma Kilosa, wakati kamati hiyo ilipokagua maendeleo ya ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR, Mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akitoa maelekezo kwa Meneja Mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro, Mhandisi Machibya Masanja, wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilipotembelea na kukagua mataruma yanayozalishwa katika Kiwanda cha Kilosa, Mkoani Morogoro.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso (wa pili kushoto) akiwa na wajumbe wa kamati hiyo,wakimsikiliza Mhandisi wa Udhibiti Ubora kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mhandisi Ezekiel Abel, akitoa maelezo ya namna kiwanda cha mataruma Kilosa kinavyozalisha mataruma, wakati kamati hiyo ilipokagua maendeleo ya ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR, Mkoani Morogoro.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa, akifafanua jambo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso (wa pili kulia) na wajumbe wa kamati hiyo, wakati ilipokagua maendeleo ya ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR, Mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, na moja ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mheshimiwa Charles Kitwanga, ndani ya treni ya majaribio ya SGR, wakati kamati hiyo ilipokagua maendeleo ya ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR, Mkoani Morogoro.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Wizara na Shirika la Reli Tanzania (TRC) katika mlango wa tanuru la reli, wakati kamati hiyo ilipokagua maendeleo ya ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR, Sehemu ya Makutupora-Dodoma, Mkoani Morogoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...