Mapema leo 30/03/2020 katika Uwanja wa Mazoezi wa Kikosi cha kutuliza
Ghasia Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi La Polisi CP
Liberatus Sabas, ameongea na Askari wa Vikosi Maalum kutoka mikoa
mbalimbali waliowasili mkoani Mtwara kwaajili ya kuimalisha Ulinzi
katika mpaka ya Tanzania na Msumbiji baada ya kutokea machafuko nchini
humo.
Kamishna wa Opereshni na Mafunzo CP Liberatus Sabas, akikagua moja ya
silaha aina ya Mota ambayo itatumika katika Operesheni ya kuimalisha
ulinzi katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji baada ya Nchini humo
kuvamiwa kwa kambi za Jeshi na vituo vya Polisi pamoja na Mabenki nchini
Msumbiji siku ya tarehe 23/03/2020.
Kamishna wa Opereshni na Mafunzo CP Liberatus Sabas, akiwatia Moyo
Askari waliopangwa kufanya Doria maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mtwara
baada ya kutokea kwa uvamizi wa vituo vya Polisi, Kambi za Jeshi na
Mabenki huko nchini Msumbiji. (PICHA NA JESHI LA POLISI)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...