Mkurugenzi wa Yono Auction Mart Scolastica Kevela akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati akizindua mfumo wa mnada mtandaoni.
 Mtalaam wa mifumo wa Kampuni ya Yono Auction Mart Jordan Mwaisango akielezea namna mfumo wa mnada mtandaoni unavyofanya kazi na hasa jinsi wanunuzi na wauzaji wanavyoweza kuutumia

Na Said Mwishehe,Michuzi Blogu ya jamii


KAMPUNI ya udalali ya Yono Auction Mart imezindua mfumo wa mnada mtandao ambao ni maalum kwa ajili ya kuwawezesha wanunuzi na wauzaji wa bidhaa mbalimbali kupata mahitaji yao bila kupata usumbufu wowote.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Machi 16, mwaka 2020 wakati wa uzinduzi wa mnada huo, Mkurugenzi wa Yono Scolastica Kevela amesema pamoja na mambo mengine kuzinduliwa kwa mnada huo kutaiwezesha Serikali kupata mapato yake kwa uhakika tofauti na hapo nyuma kutokana na watu wengi kuingilia shughuli za udalali pasipo kufuata utaratibu.

Ameongeza kuwa hatua ya kampuni hiyo kuzindua mnada mtandao huo, umekuja siku chache baada ya Kampuni hiyo kukabidhiwa leseni na utoaji wa huduma hizo kutoka Wizara ya Gedha iliyowapa mamlaka wao kama madalali wa siku nyingi kuongeza tija katika majukumu yake.

“Kuzinduliwa kwa mnada huu haina maana kuwa tutasitisha minada ya awali ambayo kampuni ilikuwa ikiifanya, bali kutazidi kutazidi kuongeza tija kwa wateja wetu wenye nia ya kutaka kununua au kuuza bidhaa kutoka katika kampuni yetu,” amesema Scolastica

Ameeleza kuwa mtarajio yao baada ya kuzinduliwa kwa mnada huo pamoja na kuwanufahisha wateja wa hapa nchini, pia kutatoa fursa kwa wateja walioko nje ya nchi kushiriki na kujipatia bidhaa mbalimbali zikiwemo nyumba na magari na hivyo kuwaepusha na malalamiko ya kudhurumiwa fedha zao kutoka kwa baadhi ya watu wakiwemo ndugu zao.

Amesema mnada huo kwa njia ya kielekitroniki unaopatikana kupitia tovuti ya www.yonobid.co.tz, pia utatoa fursa kwa wananchi mbalimbali wanaotaka kuuza bidhaa zao kushiriki bure katika kipindi cha miezi mitatu na baada ya hapo wataweka utaratibu wa kuchangia kiasi kidogo cha gharama kwa ajili ya uendeshaji.

Pia uamuzi wa kunzishwa kwa mfumo huo, amesema umelenga kutekeleza mpango kabambe wa Serikali ya awamu ya tano ambapo Wizara , idara, wakala na taasisi za serikali pia zimetakiwa kuendesha shughuli zake hasa za ukusanyaji wa mapato ya serikali kwa kutumia mfumo wa kielektroniki.

Kwa upande wake Mtaalam wa mifumo wa Kampuni hiyo Jordan Mwaisango amesema ujio wa mfumo huo pamoja na mambo mengine utarahisisha shughuli za minada huku akisisitiza kikubwa anachopaswa kufanya mhitaji ni kujisajili na mfumo huo ili aweze kuutumia.

"Kujiunga na mfumo huo ni rahisi kwa mtu yoyote kikubwa anapaswa kuwa na ‘simu janja’ kompyuta au Ipad itakayomwezesha kuingia moja kwa moja na kufanya mchakato huo,"amesema Mwaisango huku akitoa rai kwa Watanzania kutumia mfumo huo katika kuuza au kununua bidhaa mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...