Jeshi
la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia FESTO
MADUHU [28 -30] Mbeba Mizigo @ Kuli na Mkazi wa Mtaa wa Benki Kabwe Jijini
Mbeya kwa tuhuma za kumuua mpenzi wake na kisha yeye mwenyewe kujaribu kujiua
kwa kisu.
Ni
kwamba mnamo tarehe 22/03/2020
majira ya saa 09:00 Asubuhi huko
katika nyumba ya kulala wageni iitwayo “NEGERO”
iliyopo Mtaa wa Ilolo, Kata ya Ruanda, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya katika
chumba namba 111 @ Victoria, Mwanamke mmoja aitwaye JESCA MICHAEL @ KUNGULU [28] Mhudumu wa Nyumba ya Kulala Wageni na
Baa na Mkazi wa Ilolo Jijini Mbeya aligundulika kuuawa kwa kukabwa shingo na
kupigwa sehemu za usoni na mtuhumiwa FESTO
MADUHU ambaye ni mpenzi wake.
Kiini
cha tukio hili ni wivu wa kimapenzi kwani mtuhumiwa alikuwa anamtuhumu marehemu
kuwa alikuwa na mahusiano na mwanaume mwingine ambaye jina linahifadhiwa kwa
sababu za kiupelelezi na ufuatiliaji.
Katika
ufuatiliaji wa kumkamata mtuhumiwa mara baada ya tukio hilo, mtuhumiwa alikutwa
akiwa amejifungia nyumbani kwake na baada ya askari kuvunja mlango wa nyumba
hiyo alikutwa akiwa anaendelea kujichinja koromeo lake kwa kutumia kisu ambapo
askari Polisi walimuokoa na kumpeleka Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa
matibabu.
Mwili
wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa uchunguzi zaidi
wa kitabibu. Aidha mtuhumiwa anaendelea kupatiwa matibabu kitengo cha dharura
Hospitalini hapo akiwa chini ya ulinzi na mara apatapo nafuu atahojiwa na
kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma za Mauaji na kujaribu kujiua.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi ULRICH MATEI anatoa wito kwa jamii
kuacha kujichukulia sheria mkononi. Aidha anatoa wito kwa jamii kuacha tabia ya
kupuuzia migogoro ya aina yoyote baina ya mtu na mtu au kikundi cha watu na
badala yake watoe taarifa mapema sehemu husika likiwemo Jeshi la Polisi kwa
hatua zaidi za kisheria.
Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI -SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...