Na Amiri kilagalila,Njombe
Mkuu wa Gereza la Ndulamo
wilayani Makete mkoani Njombe amewaomba wadau mbali mbali kujitokeza kusaidia
ukamilishwaji wa ujenzi wa zahanati ya gereza hilo ili kuokoa maisha na
kuimarisha usalama kwa wafungwa na mahabusu ndani ya gereza.
Gereza la wilaya ya Mkete
(Ndulamo) lililopo wilayani Makete, ni moja kati ya magereza yanayopatikana
ndani ya mkoa wa Njombe.Moja ya changamoto kubwa hapa inayoelezwa na Aloyce
kayela mrakibu mwandamizi wa magereza wilaya ya Makete ni kukosekana kwa huduma
za afya kwa mahabusu na wafungwa wanaotumikia adhabu zao ndani ya gereza hili
hususani pale wanapougua ghafla nyakati za usiku.
“kwa hiyo baada ya kukaa na
kamati yangu tukabuni na kujitolea ngvu zetu kujenga zahanati ya ndani ambapo
wafungwa au mahabusu watakapopata maradhi ya ghafla basi watahudumiwa ndani ya
gereza”alisema
Magereza ni pahala ambapo
watu huifadhiwa pindi wanapokiuka na kwenda kinyume na sharia za nchi lengo
likiwa ni kujifunza na kurekebisha tabia zao.
Kwa kutambua umuhimu wa
kuendelea kuwajali na kuwathamini kama watu wa kawaida,chama cha maendeleo
wilayani Makete MDA wamejitolea mifuko ya saruji 40, Bati 40 na misumari,tayari
kwa kuendelea na ujenzi wa zahanati ya gereza la Ndulamo.
“kwa hiyo tunaamini walihapa
nao wana nafasi kubwa ya kutumikia nafasi zao za gereza lakini siku moja tuje
kuungana nao kuleta maendeleo kwenye wilaya yetu kwahiyo huku ni lazima waweze
kupata hata huduma za afya waweze kutoka salama”alisema Mpandila
Mwenyekiti wa kamati ya
ulinzi na usalama wilaya ya makete Veronica Kessy ambae ni Mkuu wa wilaya hiyo
amesema kunahaja ya wadau kuendelea kujitokeza katika kusaidia ujenzi wa zahanati
hiyo huku akiwapongeza viongozi na wanachama wa MDA kwa kutambua umuhimu wa
zahanati hiyo.
“tayari mmeleta mabato
arobaini,mifuko ya simenti arobaini mmeleta misumari nichukue nafasi
kuwapongeza wana M.D.A na ninapata faraja kwamba mpo kwa ajili ya Makete”alisema
Veronika Kessy
Aloyce Kayera Mkuu wa
Gereza la ndulamo wilaya ya makete amepokea baadhi ya vifaa vilivyotolewa na
chama cha maendeleo makete MDA huku akiwapongeza kwa kuguswa na kutoa kile
walichojaaliwa.
Vile vile chama cha
maendeleo Makete wamekabidhi fedha kiasi cha shilingi milioni moja na laki
mbili kwa ajili kuhakikisha umeme unafika katika nyumba za walimu wa shule ya
sekondari ya wasichana Makete.
Mkuu wa wilaya ya Makete Veronica Kessy pamoja na viongozi wa chama cha
maendeleo Makete wakionesha moja ya msaada uliotolewa na wanachama wa chama cha
maendeleo makete M.D.A
Zahanati
ya magereza Makete inayosaidiwa baadhi ya vifaa kwa ajili kukamilisha ujenzi
Mkuu
wa wilaya ya Makete Veronica Kessy wakati akizungumza kabla ya kupokea msaada.
Katibu
wa chama cha maendeleo Makete Award Mpandila akizungumza kabla ya kukabidhi
msaada wa bati misumari na mifuko ya saruji
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...