WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema mwishoni mwa mwezi Machi, 2020 Serikali
inatarajia kusaini mkataba wa ujenzi wa barabara ya Nanganga-Ruangwa
yenye urefu wa kilometa 50 kwa kiwango cha lami.
Hatua
hiyo itawezesha kutatuliwa kwa kero ya changamoto ya miundombinu ya
barabara inayowakabili wananchi wa wilaya ya Ruangwa kwa muda mrefu.
Waziri
Mkuu alitoa kauli hiyo jana jioni (Jumamosi, Machi 14, 2020) wakati
akizungumza na wananchi wa wilaya ya Ruangwa kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika katika uwanja wa Wandorwa.
Alisema
barabara hiyo ambayo kwa sasa haipo katika hali nzuri itajengwa kwa
kiwango cha lami na kwamba Serikali imejipanga katika kuboresha
miundombinu ya barabara kwenye maeneo mbalimbali nchini.
Pia,
Waziri Mkuu aliwataka wananchi hao washirikiane katika shughuli za
maendeleo na kuweka kando itikadi zao za kisiasa kwa sababu maendeleo
hayana chama.
“Mimi
nitaendelea kuwatumikia, kuwasikiliza na kuwahudumia, nawaomba
tushirikiane na tuweke kando masuala ya itikadi za vyama, huu ni wakati
wa kazi ni bora tukashirikiana kufanya kazi kwa maendeleo ya Ruangwa
jambo ambalo linawezekana.”
Kwa upande wao,
wananchi walitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Awamu ya Tano
inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwajali na kwamba
ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami ni mkombozi kwao.
Walisema
awali katika wilaya yao walikuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali
zikiwezo za upatikanaji wa huduma za afya, maji na elimu lakini kwa sasa
ni historia kwani Serikali ilishazitatua na ilibaki ya barabara ambayo
nayo inakwenda kuwa historia.
“Tunamshukuru
Rais wetu Dkt. Magufuli kwa upendo wake hasa kwa sisi wanyonge,
tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu yeye pamoja na wanaomsaidia waweze
kutimiza malengo yao yakiwemo na ya ujenzi wa barabara yetu kwa kiwango
cha lami.” Alisemma Mwanajuma Chikambo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...