Na Karama Kenyunko-Michuzi Blog.

MASENETA sita kutoka nchini Ufaransa wako nchini Tanzania kwa ziara za kikazi ambapo wanatarajia kutembelea mikoa mbalimbali pamoja na visiwani Zanzibar kujionea shughuli za maendeleo zinazofanywa na wadau wanaonufaika na misaada ya Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD).


Ziara hiyo itafanyika kwenye Mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha na kwamba ni matokeo ya ziara iliyofanywa Septemba mwaka jana na marafiki wa Ufaransa na Tanzania na kuazimia kufanya mdahalo utakaowahusisha wadau wa maendeleo ngazi ya jamii na wawakilishi wa nchi mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo Machi 2,2020, Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier alisema maseneta hao na wilaya wanazotoka kwenye mabano wanaongozwa na kiongozi wa msafara huo, Rais wa Kamati ya Bunge ya Mipango Miji na Maendeleo Endelevu, Herve Maurey (Eure) na Marta de Cidrac (Yvelines).

Wengine ni Franciise Ramond (Eure-et-Loir), Joel Bogot (Maine-et-Loire), Jerome Bignon (Somme) na Guillaume Gontard (Isere) ambao wameanza ziara hiyo visiwani Zanzibar Machi Mosi na itahitimishwa kwenye uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) Machi 8 mwaka huu.

Alisema shirika hilo la AFD limetumia zaidi ya Euro milioni 760 kusaidia maendeleo endelevu kwenye sekta ya Maji, Nishati na Afya nchini Tanzania fedha zilitolewa kwa awamu kuanzia mwaka 2009 hadi 2019.


"Mdahalo huo mkubwa unaitwa 'Africa-France Summit 2020' utafanyika Juni 4 hadi 6 mwaka huu kwenye jiji la Bordeaux huko Ufaransa, utakuwa fursa nzuri kwa wadau na serikali zao kusikia na kupata uzoefu wa nchi nyingine," alisema Balozi Clavier.


Akizungumzia ziara hiyo ya siku saba, Seneta Maurey alisema watatembelea na kuzungumza na wakuu na watumishi wa taasisi zinazonufaika na misaada ya AFD ili kuona namna sahihi ya kuendelea kufadhili miradi husika na changamoto wanazokabiliana nazo kwenye utendaji wao.

Alidema wakiwa Morogoro tutatembelea Shirika la Kilimo Endeleo Tanzania (SAT), ambao wanashirikiana na ubalozi huo kufanya mradi wa kilimo ikolojia wakiwa na Mamlaka ya Maji safi na Maji taka Mji wa Morogoro (MORUWASA).


Alisema wakiwa Arusha watatembelea Mamlaka ya Eneo la Wanyamapori (WMA) zilizopo ukanda wa Mbuga ya Taifa ya Tarangire na jijini Dodoma watazungumza na Meya Davis Mwamfupe wakimkaribisha kwenye mkutano wa Juni huku wakizingatia kuwa ni mji unaokua hivyo kuhitaji mpango bora wa makazi ya kisasa.

Kwa mujibu wa Seneta Maurey, watazungumza pia na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangwala kuona namna bora ya kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi na maendeleo ya wanyamapori na utalii endelevu.
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Fr'ed'eric Clavier(wa tatu kulia) akiwa na maseneta sita kutoka nchini Ufaransa ambao wamekuja nchini kwa ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Fr'ed'eric Clavier( kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika leo Machi 2 mwaka 2020.Kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya Mipango Miji na Maendeleo Endelevu nchini Ufaransa Herv'e Maurey
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Fr'ed'eric Clavier(wa kwanza kulia) akiteta jambo na Mwenyekiti wa kamati ya Mipango Miji na Maendeleo Endelevu nchini Ufaransa Herv'e Maurey wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa kamati ya Mipango Miji na Maendeleo Endelevu nchini Ufaransa Herv'e Maurey akizungumza wakati wa mkutano wa waandishi wa habari na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Tanzania Fr'ed'eric Clavier. Mwenyekiti huyo ni miongoni mwa ujio wa maseneta sita wa nchi hiyo ambao wapo nchni.
Seneta Marta de Cidrac(kushoto) akiteta jambo na Seneta J'ero'me Bignon wakati wa mkutano huo ambao pamoja na mambo mengine Ufaransa imeeleza ilivyojipanga kuendeleza ushirikiano kati yake na Serikali ya Tanzania
Seneta Marta de Cidrac(wa kwaza kulia) akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Tanzania Fr'ed'eric Clavier(wa tatu kutoka kulia) akiwa na maseneta sita kutoka nchini Ufaransa ambao wako nchini kwenye ziara ya kikazi.Wa nne kulia ni Ofisa wa Mawasiliano wa Ubalozi wa Ufaransa nchini
Seneta Marta de Cidrac(kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Fr'ed'eric Clavier( kulia) akiwa na Mwenyekiti wa kamati ya Mipango Miji na Maendeleo Endelevu nchini Ufaransa Herv'e Maurey wakisikiliza maswali kutoka kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Fr'ed'eric Clavier( kulia) akijibu moja ya swali la waandishi wa habari.
Maseneta sita kutoka nchini Ufaransa, Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania wakiwa na waandishi wa habari katika meza ya pamoja wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.(PICHA NA SAIDI MWISHEHE-MICHUZI BLOG )


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...