Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew
Massawe (kulia) akizungumza wakati wa Mkutano wa Makatibu Wakuu, Maafisa
Waandamizi na Wadau wa Utatu wa sekta ya Kazi na Ajira wa Nchi
Wananchama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuelekea
Mkutano wa Mawaziri wa sekta hiyo utakaofunguliwa rasmi na Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Machi 5, 2020 Jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Naibu Katibu Mtendaji mwenye dhamana ya Utangamano wa
Kikanda, Dkt. Thembinkosi Mhlongo.

Wawakilishi
kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa
Afrika (SADC), wakifuatilia ajenda zilizokuwa zikiwasilishwa katika
Mkutano wa Makatibu Wakuu, Maafisa Waandamizi na Wadau wa Utatu wa SADC
sekta ya Kazi na Ajira uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Mwakilishi kutoka
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo akichangia hoja wakati wa Mkutano wa
Makatibu Wakuu wa sekta ya Kazi na Ajira wa SADC ikiwa ni hatua za
kuelekea katika Mkutano wa Mawaziri na Wadau wa Utatu wa Sekta ya Ajira
na Kazi wa SADC, utakaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa
Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew
Massawe (kulia), akifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na mwakilishi
kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. (Wa pili kutoka kulia) ni Naibu
Katibu Mtendaji mwenye dhamana ya Utangamano wa Kikanda, Dkt.
Thembinkosi Mhlongo, Mkurugenzi wa Huduma za Kijamii na Rasilimali Watu
SADC Bi. Duduzile Simelane naMwakilishi wa Sekretarieti ya SADC, Bw.
Maxwell Parakokwa.

Baadhi ya Maafisa
Waandamizi kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakifuatilia Mkutano huo.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...