AJALI YA GARI KUGONGA BAJAJI NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU WAWILI.

JESHI la Polisi mkoani Mbeya linamshikilia Dereva AYOUB BALENZI MWANDWANGWA [36] Mkazi wa Ilomba Jijini Mbeya ambaye ni Dereva wa Basi la RAHABU linalofanya Safari zake kati ya Mbeya – Ifakara Morogoro kwa kosa la kusababisha vifo kwa dereva wa Bajaji ambaye bado hajafahamika jina na abiria wake aitwaye ESTER MBOJE [35] Mkazi wa Ilemi.
Ni kwamba mnamo tarehe 24/03/2020 majira ya saa 06:15 asubuhi huko Ilomba, Kata ya Ilomba, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya katika barabara kuu ya Mbeya kwenda Iringa, Gari namba T.413 AVU aina ya Scania Basi la RAHABU likitokea Mbeya kuelekea Ifakara wakati lina “overtake” bila kuchukua tahadhari na kwa makusudi alizidi upande wa kulia wa barabara na kwenda kugonga Bajaji MC 230 BGT aina ya TVS na kusababisha kupinduka kwake na kusababisha majeruhi kwa dereva wa Bajaji na abiria ESTER MBOJE [35] Mkazi wa Ilemi ambao walikimbizwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya na wakati wanaendelea kupatiwa matibabu walifariki.

Jeshi la Polisi mkoani hapa tunasikitika sana kwa ajali mbaya iliyosababishwa kwa makusudi na AYOUB BALENZI kwa kudharau usafiri wa Bajaji. Tunasema atafikishwa mahakamani kwa mauaji na tumemfutia leseni yake toka leo hii.

WITO WA KAMANDA.
Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, tunatoa rai na pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao. Nawasihi sana waendesha Pikipiki @ Bodaboda na wanaopanda/abiria wake si salama kutumia Bajaji kutoka Mafiati hadi Uyole kutokana na ufinyu wa barabara na pia magari makubwa wanatumia kwenda mpaka nje ya nchi [Transit]

Aidha Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linawasihi mamalaka zinazohusika kutengeneza barabara za michepuko katika kiwango ili Pikipiki @ Bodaboda na Bajaji ziweze kuzitumia ili Speed ya magari makubwa iongezeke na kupita haraka katikati ya Jiji letu.

KUSAFIRISHA MAZAO NJE YA NCHI BILA KIBALI.

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya BWAKISA BROWN [22] mkazi wa Njisi Wilayani Kyela kwa tuhuma za kusafirisha bila kibali mahindi makavu magunia 60 kwenda nchini Malawi.
Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 23.03.2020 majira ya saa 23:45 usiku huko Kivuko cha Kasumulu, Kata ya Ikimba, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya baada ya Jeshi la Polisi Mkoani hapa kwa kushirikiana na Maafisa wa TRA kupata taarifa na kuweka mtego na kufanikisha kumkamata mtuhumiwa akiwa na Mahindi hayo. Mahindi yamekabidhiwa Idara ya Forodha kwa hatua zaidi za kisheria.

KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WA WIZI WA MIFUGO. 

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili ROBERT SHABANI [20] na OMARY MASANJA [24] wote wakazi wa Mamba wakiwa na Ng’ombe kumi [10] wa wizi.
Watuhumiwa walikamatwa mnamo tarehe 23.03.2020 majira ya saa 06:30 asubuhi baada ya Jeshi la Polisi mkoani hapa kupata taarifa na kufanya msako mkali huko Kijiji na Kata ya Lupatingatiga, Tarafa ya Kipembawe, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya. Watuhumiwa walikamatwa wakiwa na Ng’ombe kumi wenye thamani ya Tsh. 4,000,000/= mali ya SAIMON CHAPULA [65] mkazi wa Mawelu ambaye aliripoti kuibiwa Ng’ombe hao na mara moja Jeshi la Polisi lilianza msako na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wakiwa na Ng’ombe hao. Upelelezi unaendelea.

Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...