Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
MCHEKESHAJI
maarufu na mkongwe kutoka Japan Ken Shimura (70) amefariki dunia usiku
wa kuamkia leo mjini Tokyo baada ya kupata maambukizi ya Corona baada ya
kupata maambukizi ya virusi vya Corona (covid 19) Shirika la Utangazaji
CNN na watu wake wa karibu wamethibitisha.
imeelezwa
kuwa Shimura aliumwa homa ya mapafu kufariki dunia jumapili usiku, huku
ikielezwa kuwa alianza kusikia dalili ikiwemo uchovu Machi 17 na
alilazwa Machi 20 kabla ya kugundulika kuwa na virusi hivyo Machi 23
mwaka huu.
Shimura alianza shughuli ya uchekeshaji mwaka 1974 akiwa kivutio kwa wajapani wengi kupitia kundi la "Drifters".
Japan kupitia Wizara ta afya imetangaza visa 173 vya virusi vya Corona (covid 19) huku visa 68 vikitokea Tokyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...