Naibu
Waziri wa Nishati Mh. Subira Mgalu akizungumza jambo kuhusiana na
mikakati ya serikali ya awamu ya tano ya kuweka mipango ya kuunganisha
nishati ya umeme wa gesi asilia katika viwanda vipya 50 wakati wa ziara
ya Kamati ya kudumu ya bunge ya nishati na madini ambayo ilifanya ziara
yake ya kikazi ya kutembelea baadhi ya viwanda vilivyopo katika Wilaya
ya Mkuaranga.(Picha na Victor Masangu)

Baadhi ya wabunge wanaounda kamati
ya nishati na madini wakati wanaingia katika kiwanda cha kuzalishia
chuma cha Lodhia ikiwa ni moja ya ziara yao ya kikazi kwa ajili ya
kuijionea shughuli mbali mbali zinazofanywa na wawekezaji pamoja na
kubaini changamoto zao, wa kati kati ni Mbunge wa Jimbo la Kibaha
Vijijini Hamoud Jumaa.(Picha na Victor Masangu)

Mmoja wa wakurugenzi wa kiwanda
cha Lodhia ambacho kinajishighulisha na uzalishaji wa bidhaa mbali mbali
ikiwemo chuma, akiwaonyesha wajumbe wa kamati ya bunge ya nishati na
madini jinsi ya kiwanda hicho kinavyofanya kazi pamoja na kuwaelezea
changamoto mbali mbali zinazowakabili ili kuziwasilisha kwa serikali
zifanyiwe kazi.(Picha na Victor Masangu)

Mwonekano wa mtambo maalumu wa
kuzalishia nishati ya umeme wa gesi asilia ambao umefunngwa na shirika
la TPDC katika kiwanda hicho cha kuzalishia chuma pamoja na
kutengenezea mabomba ya maj wakati wa ziara hiyo ya kamati ya bunge ya
nishati na madin.(Picha na Victor Masangu)

Baadhi ya wajumbe wa kamati ya
bunge ya nishati na madini wakiwa na viongozi mbali mbali wa kiwanda
hicho wakitembezwa katika maeneo mbali mbali ili kuweza kujionea
mwenendo mzima wa vyuma chakavu vinavyoyayushwa na kutengenezwa Nondo
mpya kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbali mbali ikiwemo ile ya
serikali.(Picha na Victor Masangu)

Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha Lodhia Haruni Lodhia ambacho kinajihusisha na uzalishaji wa kutengeneza Nondo
*************************
VICTOR MASANGU, MKURANGA
Naibu Waziri wa nsihati Subira
Mgalu alisema kwamba katika kutimiza azma ya Tanzania kuwa na uchumi wa
kati ifikapo mwaka 2025 serikali imedhamilia kusambaza na kuwaunganishia
nishati ya umeme wa gesi asilia katika viwanda vipya vipatavyo 50
ambavyo vimepitiwa na bomba la gesi ikiwemo Mkoa wa Dar es Salaam Pwani
pamoja na Mtwarana kuongeza gharama za umeme zitashuka pindi mradi wa
bwawa la umeme mwalimu nyerere utakapomalika Juni 2022 na kuzalisha mega
wati 2115.
Mgalu aliyasema hayo wakati wa
ziara ya kikazi ya kamati ya kudumu ya bunge ya nishati na Madini
ambayo yameifanya kwa lengo la kutembelea baadhi ya viwanda vilivyopo
Wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani ambavyo vinajiendesha kwa kutumia
nishati ya umeme ikiwa pamoja na kuzungumza na wawekezaji ili kubaini
changamoto wanazokabiliana nao na kuzitafutia ufumbuzi.
Naibu Waziri huyo alibainisha
kwamba kwa sasa serikali ya awamu ya tanoi mpango wake mkubwa ni
kuhakikisha inasambaza na kuviunganishia viwanda mbali mbali nishati ya
umeme ili viweze kutimiza malengo ya azma y serikali ya kuwa na uchumi
wa kati pamoja na kutoa fursa mbali mbali za ajira kwa vijana ambao ni
wazalendo lengo ikiwa waweze kujikwamua na wimbi la umasikini.
“Mpango wetu wa serikali licha ya
kuwa bado kuna baadhi ya maeneo ya viwanda hayajafikiwa na nishati ya
umeme lakini kwa sasa kupitia nishati ya gesi asilia tuna mpango wa
kuviunganishia viwanda vipya vipatavyo 50 ambavyo vipo katika Mikio ya
Dar es Salaam, Mtwara pamoja na Mkoa wa Pwani hivyo juhudi za makusudi
bado zinaendelea kwa hiyo viwanda ambavyo vinapitiwa na bomba kubwa la
gesi vitaweza kunufaika.
Aidha Naibu Waziri huyo alifafanya
kwamba pindi mradi wa umeme wa bwawa la Malimu Nyerere uliopo Wilayani
Rufiji utakapokamilika utaweza kuwa ni mombozi mkubwa kwa wawekezaji wa
viwanda vidogo, vya kati na vile vikubwa kutoka maenne mbali mbali
sambamba na kuwaunganishia wananchi wengine pamoja na taasisi za
serikali na sizozo za serikali.
Katika hatua nyingine Mgalu
ameipongeza kamati ya kudumu ya bunge ya nishati na madini kwa kuweza
kwenda kutembelea katika kiwanda cha kuzalisha chuma pamoja na mabomba
ya maji ili kuweza kubainichangamoto mbali mbali ambazo zinawakabili
wawekezaji na hatimaye kuweza kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu ambao
utasaidia kutimiza azma ya serikali ya kuwa na uchumi wa kati kupitia
viwanda hivyo.
Kwa upande wake Kaimu mwenyekiti
wa kamati ya kudumu ya bunge ya nishati na Madini Vedastus Matayo
alibainisha kwamba ujenzi wa kiwanda hicho utaweza kuipunguzia serikali
gharama kubwa ambazo zimekuwa zikitumia kwa ajili ya kuagiza baadhi ya
Nondo kutoka nje ya nchi hivyo amempongeza mwekezaji huyo kwa kuwekeza
katika Wilaya ya Mkuranga kwani kumesaidia vijana zaidi ya 1 300 kupata
fursa ya ajira.
“Sisi kama kamati kwa kweli
tunapenda kumpongeza mwekezaji huyo kwa kuweza kuwekeza katika Wilaya ya
Mkuranga ambayo ipo katika Taifa letu ya Tanzania hii ni hatua nzuri
ambayo ameifanya na kwa sasa anazalisha bidhaa mbali mbali kwa kutumia
nishati ya umeme wa gesi asilia hivyo kutaweza kuleta mabadiliko chanya
ya kimaendeleo kwa wananchi wenyewe pamoja na wale wawekezaji wa ndani
na nje ya nchi,”alibainisha Matayo
Aidha Matayo katika hatua nyingine
alibainisha kuwa Kamati ya bunge ya nishati ya kudumu ya nishati na
madini ilibaini kuwepo kwa urasimu na ucheleweshaji wa vibali kutoka
kwa baaadhi ya mamlaka zinazohusika kwa wawekezaji wa sekta ya viwanda
pamoja na gharama ya nishati ya umeme kuwa ni kubwa hivyo hivyo
watayachukua mapendekezo hayo kwa ajili ya kuyawasilisha bungeni ili
serikali iweze kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu.
Pia alisema kuwa mapendekezo
pamoja na changamoto mbali mbali ambazo wamekutana nazo katika kiwanda
hicho ikiwemo na maeneo mengine ambayo tayari wameshayapitia
watayawasilisha serikalini ili yaweze kufanyiwa kazi ikiwemo na kutilia
mkazo katika suala la usumbufu mkubwa wanaoupata wawekezaji pindi
wanapohitaji kuagiza matilio mbali mbali kutoka nje ya nchi kwa ajili ya
kutengeneza bidhaa zao.
Awali akitoa taarifa mbele ya
Kamati ya nishati na madini Mkurugenzi mtendajiwa wa kiwanda hicho cha
kuzalisha chuma Haluni Lodhia amebainisha kwamba hapo awali walikuwa
wanakabilia na changamoto kubwa ya ukosefu wa nishati ya umeme wa
uhakika pamoja na miundombinu ya barabara,ambapo ameipongeza serikali ya
awamu ya tano kupitia Shirika la maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)
kwa litafutia ufumbuzi suala hilo na hatimaye kuanza utekelezaji wa
kuzalisha bidhaa mbali mbali, ikiwemo Nondo, mabomba ya maji na bodi za
jasi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...