Naibu Waziri Wa Kilimo, Ambaye Pia Ni Mbunge Wa Morogoro Kusini Mashariki Mhe Omary Tebweta Mgumba,Akiongea Na Viongozi Pamoja Na Wananchi Wa Kijiji Mfumbwe Akiwa Katika Ziara Yake Ya Kukagua Miradi Ya Maendeleo Katika Kata Ya Mkuyuni Halmashari Ya Morogoro Vijijini.
.Wananchi Wa Kijiji Cha Kibwaya Kata Ya Mkuyuni Halmashauri Ya Morogoro Vijijini akimsikiliza Mbunge Wao Wa Morogoro Kusini Mashariki Ambaye Pia Ni Naibu Waziri Wa Kilimo Mhe Omary Tebweta Mgumba(Hayupo Pichani) Wakati Wa Ziara Yake Ya Kukagua Miradi Ya Maendeleo Katika Kata Hiyo.
Mbunge Wa Jimbo La Morogoro Kusini Mashariki Na Naibu Waziri Wa Kilimo Mhe Omary Tebweta Mgumba Akiambana Na Viongozi Wa Kata Ya Mkuyuni Na Kijiji Cha Mfumbwe Wakati Wa Ziara Yake Ya Kukagua Miradi Ya Maendeleo Katika Kata Ya Mkuyuni
Diwani Wa Viti Maalumu Kata Ya Mkuyuni Mhe Asha Ally Akiongea Na Wananchi Wa Kijiji Cha Mfumbwe Wakati Wa Ziara Ya Mbungu Wa Jimbo La Morogoro Kusini Mashariki Na Naibu Waziri Wa Kilomo Mhe Omary Tebweta Mgumba. ………………………………………………………………………………………………………………….
Na Farida Saidy Morogoro Jamii Imetakiwa Kuunga Mkono Kwa Vitendo Juhudi Zinazofanywa Na Serikali Ya Awamu Ya Tano Inayongozwa Na Rais Dkt John Pombe Magufuli Kwa Kuitunza Na Kuilinda Miradi Ya Maendeleo Inayotekelezwa Katika Maeneo Yao Na Kutoa Taarifa Kwa Mamlaka Husika Pale Wanapoona Kunasitofahamu Au Kusuasua Kwa Miradi Hiyo.
Hayo Yamesemwa Kwa Nyakati Tofauti Na Naibu Waziri Wa Kilimo, Ambaye Pia Ni Mbunge Wa Morogoro Kusini Mashariki Mhe Omary Tebweta Mgumba Alipofanya Ziara Katika Kata Ya Mkuyuni Jana March 2, 2020,Kwa Lengo La Kukagua Miradi Ya Maendeleo Inayotekelezwa Katika Kata Hiyo Na Kuzungumza Na Wananchi.
Mhe Mgumba Amesema Serikali Inafanya Kazi Kumbwa Sana Kutekeleza ,Miradi Ya Maendeleo Katika Jimbo La Morogoro Kusini Mashariki Na Tanzania Kwa Ujumla Hivyo Amewataka Wananchi Kuitunza Na Kuilinda Kwani Miradi Hiyo Ni Ya Wananchi Na Sio Ya Mbunge Wala Rais.
Hata Hivyo Aliwata Wananchi Kuendelea Kujitolea Katika Kuchangia Mradi Mbalimbli Ikiwemo Ya Miundombinu Ya Barabara Pamoja Na Ile Ya Elimu Ili Kusaidia Kukuza Uchumi Wao Na Taifa Kwa Ujumla.
“Kwani Madalasa Yale Yakijengwa Atakuja Kusoma Mtoto Wa Magufuri Au Mgumba?,Si Watasoma Watoto Wa Kibwaya? Au Nadanganya Ndugu Zangu?” Aliuza Mgumba.
Awali Wakitoa Kelo Kwa Mhe Mbunge Na Naibu Waziri Wa Kilimo, Wananchi Wa Kijiji Cha Kibwaya Wamemuomba Mhe Mgumba Kufuatalia Sitofahamu Iliyoko Katika Maradi Wa Maji Wa Mseleleko Wenye Thamani Ya Mia Sita Na Kumi Millioni Laki Saba Na Mia Tisa Ambao Unatekelezwa Katika Kijiji Hicho,Huku Ukijengwa Chini Ya Kiwango Hali Inayosababisha Mabomba Kupasuka Na Tank Kuwa Na Nyufa.
Katika Hatua Nyingine Mhe Mgumba Akiwa Katika Kijiji Cha Mfumbwe Ameuagiza Ungozi Wa Kijiji Hicho Kubomoa Na Kujenga Upya Madalasa Yaliokuwa Chakavu Katika Shule Ya Msingi Mfumbwe Ambayo Inauhaba Wa Vyumba Vya Madalasa Na Kusema Kuwa Atashirikiana Na Serikali Ya Kijiji Kuhakisaha Watoto
Hawasomi Chini Ya Miti,Sambamba Na Kuishukuru Bank Ya Nmb Kwa Kutoa Mabati Mia Moja (100) Katika Shule Katika Ziara Hiyo Ya Siku Moja Mhe Mgumba Amepata Nafasi Ya Kutembelea Na Kujionea Miradi Mbalimbali Ya Mendeleo Inayotekelezwa Katika Kata Hiyo Ikiwemo Ya Elimu,Afya Na Maji, Pamoja Na Kuongea Na Wananchi Wa Vijiji Vya Mfumbwe,Kibwaya,Na Kivumi Ambapo Shughuri Yao Kumbwa Ya Kiuchumi Ni Kilimo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...