Miche ya zao la korosho ambayo imeonekana kustawi vizuri ambapo kwa kuanza mkoa wamezalisha miche laki sita  na kusambaza kataika maenza mkoa wa Katavi
 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Komredi Juma Homera 

Zao la pamba ambalo linaonekana kukubali katika ardhi ya katavi na linalotarajia mwaka huu  kuchakatwa Mkoani Katavi

zao la ufuta ambalo ni moja wapo ya zao lililoingia katika mfumo wa stakabadhi ghalani


Na. Josephine mallango 

Mkoa wa Katavi kuleta mapinduzi ya kilimo kwa mazao ya kibiashara nchini  ,korosho na pamba zashika kasi huku ufuta, alizeti na karanga zikiingia rasmi katika mfumo wa stakabadhi ghalani .

Katavi ni moja kati ya mikoa michache ya Tanzania iliyobaki yenye ardhi ya kujivunia yenye rutuba ya kutosha ambayo unalima mazao na mavuno ya tija na ziada bila kuwepo kwa matumizi ya mbolea huku changamoto za visumbufu vya mazao ni chache na zinatatulika ukilinganisha na mikoa mingine nchini . 

Mkoa wa Katavi umejiwekea Mazao ya kimkakati ,wakulima waliozoea kulima zao la kibiashara la tumbaku wanaona fulsa ya kutumia mazao ya pamba na korosho kuongeza wigo na tija kutokana na mazao hayo kuwa na ustawi mzuri katika ardhi ya Katavi yenye rutuba ya kutosha .

Mkuu wa mkoa wa katavi komredi Juma Homera amesema Kupitia mpango huo wa mazao ya kimkakati mkoa umeweza kupanda miche ya zao la korosho zaidi ya laki 600,000.kwenye eneo la hekari elfu 32,000. kwa awamu ya kwanza 2019/2020 na wanatarajia kwa msimu wa 2020/2021 kuotesha miche milioni 1,000,000. itakayopandwa katika eneo la hekari elfu 35,000. na tayari wameshapa wawekezaji. 

Kwa upande wa zao la Pamba amesema huu ni msimu wa tatu na uzalishaji wake umevuka lengo kutoa tani 500 msimu wa kwanza 2017/2018 kufikia tani elfu 8000 kwa msimu wa 2018/2019 na kwa msimu 2019/2020 wanatarajia kufikia tani elfu 29,000. Au 30,000 na pamba inayozalishwa katika Katavi ina ubora wa hali ya juu kutokana na ardhi kuwa na rutuba.

’’ uzalishaji wa pamba mkoani katavi unakwenda kufikia kile kiwango cha kilimo cha pamba kinachotakiwa heka moja kuzalisha tani moja, kwa sasa wakulima wanatoa kilo 800 mpaka 1200 kwa heka wakati katika mikoa ya kanda ya ziwa wakulima wa pamba wengi wao wanatoa kilo 300 mpaka mia 600 kwa heka , na bado changamoto katika zao la pamba katavi bado chache zinatatulika tofauti na katika mikoa mingine hali hiyo ndio inaongeza uzalishaji wa pamba katavi’’ Komredi Homera .

Uzalishaji huo wa tija kwa muda mfupi umepelekea mkoa wa Katavi kupitia wilaya ya Tanganyika kuteuliwa na wizara na bodi ya pamba kuwa kitaru cha taifa cha kuzalisha mbegu na kusambaza nchini na kwamba ni fahari kwa wanakatavi kuteuliwa na kupewa jukumu la kuhudumia nchi .

Komredi Homera amesema mazao yote hayo yanatanguliwa na mazao makubwa mahindi na mpunga ,mahindi kwa msimu wa 2018/2019 uzalishaji mavuno zaidi ya tani laki 300,000. , na msimu huu wa 2019/2020 wanatarajia uzalishaji mavuno yatavuka lengo na kufikia tani 500,000 ambapo watasambaza ziada kwa mikoa itakayokuwa na upungufu wa chakula nchini ,mpunga mavuno tani laki 300,000 kwa msimu wa 2018/2019 ambapo bado kuna ziada katika maghala ya tani elfu 70 zilibaki zitaungana na mpunga wa msimu huu. 

Mkuu huyo wa mkoa ameongeza kuwa kwa sasa mkoa umejikita katika Mazao matatu yaliyoingia katika mfumo wa stakabadhi ghalani ambapo wanahimiza wakulima kujiunga na Kuuza mazao katika ushirika kutokana na kuwa na soko la uhakika kwa mkulima na mnunuzi kwa masilahi mapana kwa wakulima na kwa nchi .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...