Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere (Rufiji Hydropower Project (RHPP) umetajwa kuzidi asilimia 11 mpaka sasa na unatarajiwa kukamilika kwa wakati uliopangwa ifikapo June 2022.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka wakati wa utoaji taarifa za Mradi huo kwa Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali wanaotembelea miradi ya maendeleo hapa nchini inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Dkt. Mwinuka amesema katika utekelezaji wa mradi huo kazi kubwa ilikuwa kutoboa Miamba itakayopitisha maji ya mto ili kutoa nafasi kwa Wakandarasi kuendelea na ujenzi wa mradi, hata hivyo amewashuru Makatibu Wakuu kushiriki na kutembelea mradi huo.

“Ule Mwamba tushautoboa, hiyo ndio ilikuwa kazi kubwa na wakati wowote ndani ya mwezi mmoja au miwili ule Mto unaweza kuhama nakupita kwenye Mwamba na ujenzi ukaendelea, kila Wizara ni mdau na ana sehemu yake katika utekelezaji wake”, amesema Dkt. Mwinuka.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Msafara huo wa Makatibu Wakuu ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Prof. Sifuni Mchome amesema wameridhishwa na mradi huo kutokana na wazo lilitokana na aliyekuwa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kutokana na fursa, manufaa ya Mto Rufiji ikiwa sambamba na uzalisha Umeme, kuzuia mafuriko na uhifadhi wa mazingira.

“Ujenzi wa Viwanda unaenda sambamba na umeme unaoaminika sasa utekelezaji wa mradi huu, hata kwa Taifa kunufaika na umeme huo utakaozalishwa katika mradi huu”, amesema Prof. Mchome.

Prof. Mchome amesema mradi huo utalikomboa Taifa katika uzalishaji umeme na kuondoa tatizo la umeme hususan katika Uchumi wa Viwanda pamoja na wananchi kupata manufaa kupitia mradi huo

Naye, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Zena Said amesema lengo lakufika kutembelea mradi huo ni kutoa fursa kwa Wizara mbalimbali kutambua na kuelewa mradi huo ili kurahisisha utekelezaji wake na kukamilika kwa wakati.
 Meneja wa Mradi wa Kufua umeme wa Rufiji, Mhandisi Steven Manda akieleza juu ya utekelezaji wa mradi wa wa kufua umeme wa Rufiji kwa Makatibu Wakuu leo jijini Dar Es Salaam.


 Makatibu Wakuu na Manaibu katibu wakuu wakisikiliza kwa umakini juu utekelezaji wa mradi huu unaotarajiwa kuzalisha MW 2115.
Muonekano wa Kufua Umeme wa Rufiji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...