Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Kila ifikapo Machi 18, dunia huadhimisha siku ya magonjwa ya watoto ya Rheumatism ambayo husababishwa na hitilafu katika mfumo wa Kinga ya mwili ambayo hushambulia  sehemu mbalimbali za mwili badala ya kuulinda.

Magonjwa hayo yanaweza kusababisha ulemavu na udhaifu wa mwili.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Daktari Bingwa wa watoto kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt Francis Furia amesema magonjwa hayo huwa na madhara mengi kwa meili na husababisha ulemavu na wakati mwingine kifo.

"Walengwa wakuu katika siku hii ya leo ni watoto, vijana, wazazi na wahudumu wa afya  ambapo wazazi wanapewa elimu ili kuwahi kuwapeleka watoto hospitali mapema ili wapate matibabu na kupunguza uwezekano wa kupata madhara ya magonjwa haya ikiwemo ulemavu na vifo," amesema.

Dkt Furia amesema magonjwa haya yana changamoto kubwa ya kugundulika haraka na wengi hayana vipimo maalumu vinavyoweza kupima na kusema moja kwa moja.

"Duniani kote kuna upungufu mkubwa wa wataalamu wa kushughulikia matatizo ya Rheumatism kwa watoto na katika mwaka 2012-2019 waliweza kufanya tafiti na kupata jumla ya wagonjwa 52 ambapo katika hao watoto wanne waliweza kufariki na wengine wamepata matibabu wakiendelea nayo,"amesema.

"Kwa mwaka jana (2019) ni nchi tatu tu za Afrika walifanya maadhimisho ya siku ya Rheumatism na hili linasababishwa na ukosefu wa watalaamu wa kutambua ugonjwa huo ambapo kwa Tanzania daktari ni mmoja na Kenya ni wawili tu,"

Naye Mmoja ya waathirika wa ugonjwa wa Lupus Maureen Manyama amesema alianza kuumwa akiwa na miaka 19 ambapo ilichukua muda kidogo kufahamu kama ana tatizo hilo anashukuru kwa sas anaendelea vizuri na anawashukuru sana madaktari.

Mzazi wa Nirvan Fredy, Maureen Kiganja amesema kwa miaka mitatu amehangaika kupata tiba sahihi ya mtoto wake kwani alipimwa kila aina ya kipimo ikiwemo magonjwa kama TB lakini hakuweza kupata nafuu.

Maureen kikubwa amewaomba wazazi wakianza kuona mabadiliko ya watoto waende hospitali kupata tiba sahihi na kuwaepusha watoto hao na ulemavu au kifo.

Baadhi ya magonjwa ya Rheumatism ni ugonjwa wa viungo (Juvenile Idioaphtic Arthritis JIA), Ugonjwa wa Lupus ( System Lupus Erythrmatosus SLE), Ugonjwa wa Moyo (kawasaki Disease) , Ugonjwa wa misuli (Juvenile Dermatomyositis) na ugonjwa wa ngozi na misuli (Schleroderma).

Ugonjwa wa JIA ndio unaoshambulia watoto wengi zaidi katika magonjwa hayo. Huku ugonjwa wa Lupus ukiwa unaongoza kwenye nchi za Afrika.
 Mzazi wa Mtoto Nirvan Fredy, Maureen Kiganja akieleza changamoto alizokutana nazo kipindi ambacho alikua anamuuguza mwanae mwenye matatizo ya Rheumatism (Juvenile  Idioapthic Arthritis) kwa muda wa miaka mitatu hadi sasa ameweza kuendelea vizuri
 Daktari Bingwa wa Watoto Muhimbili, Dkt Francis Furia akizungumzia siku ya magonjwa ya watoto ya Rheunatism ambayo hufanyika kila ifikapo Machi 18 kila mwaka.
Mtoto Nirvan  mwenye matatizo ya Rheumatism ya Ugonjwa wa Viungo (Juvenile  Idioapthic Arthritis) aliyeugua kwa kipindi cha miaka mitatu na  sasa anaendelea  vizuri baada ya kupata matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...