Kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali hapa nchini ikiwemo wilaya ya Ludewa iliyopo mkoani Njombe imepelekea kufanya uharibifu wa mazao mbalimbali ikiwemo mahindi na kushusha kiwango cha uzalishaji kutoka tani laki moja na elfu kumi na moja kwa mwaka jana mpaka kufikia tani isiyozidi laki moja kwa mwaka huu
Akizungumzia suala hilo mkuu wa wilaya ya Ludewa Adrea Tsere amesema wilaya yake inaongoza kwa uzalishaji mkubwa wa zao la mahindi katika mkoa wa Njombe ambapo kwa mwaka jana ilivuna tani laki moja na elfu kumi na moja ambapo tani elfu sitini kwaajili ya matumizi ya chakula na tani 51 kwaajili ya biashara na mpaka sasa wamebakiwa na mahindi ya biashara tani 615.
Alisema wilaya hiyo ina jumla ya tarafa tano ambapo tarafa tatu amzazo ni Mlangali, Mawengi pamoja na Liganga huzalisha mahindi kwa wingi huku tarafa ya Masasi na Mwambao huzalisha mihogo na ufuta kidogo.
Alisema mvua hizi zimeleta athari katika baadhi ya maeneo ya tarafa ya mwambao ukanda wa ziwani ambao zao lao kuu ni mihogo mvua hizi zimeleta mafuriko katika mto Luhuhu na kupelekea baadhi ya mashamba ya mihogo kwenda na maji.
“Tarafa hii ya mwambao imeathirika kwa kiwango kikubwa na kusababisha upungufu wa chakuala kwakuwa watu wa ukanda huu hutegemea zaidi zao hilo kwaajili ya kupata unga n.k”, Alisema Tsere.
Aidha kwa upande wa mmoja wa wakulima hao Aliyefahamika kwa jina la Agatha Haule alisema kuwa mvua za mwaka huu zimekuwa nyingi zaidi tofauti na miaka mingine na zimekuwa na athari katika mazao yao ya mahindi pamoja na maharage.
Alisema maharage yameungua na mengine kuanza kuota kabla hayajavunwa kitu ambacho kimewaleta shida katika kutafuta masoko kwakuwa wateja wengi wanayaona hayana ubora kwakuwa yameungua.
Mkuu wa wilaya ya Ludewa, Andrea Tsere
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...