Na Grace Gurisha, Kibaha
MKUU wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi, Profesa Zacharia Mganilwa ameahidi kumpa ushirikiano muanzilishi na Mkurugenzi wa Kampuni ya kuunda magari ya BM Motor, Jonathan Nyagawa kuhakikisha mabasi aliyoyaunga yanaingia barabarani kwa kufuata utaratibu na yakiwa na ubora.

Profesa Mganilwa alitoa ahadi hayo Machi 3, mwaka huu alipofanya ziara katika Kiwanda hicho cha magari kilichopo Kibaha Madafu, Mtaa wa Zogowale eneo la viwanda la Zegeleni ambapo aliongozana na wataalamu mbalimbali kutoka katika chuo hicho lengo ni kuona kazi ambayo imefanya na Nyagawa na kumshauri.

Amesema pamoja na kwamba Shirika la Viwango Tanzania (TBS) inatoa viwango, kwa hiyo watamtaka Mkurugenzi huyo angalau awe na ripoti ya utendaji kazi ambayo ikakagua ndiyo itayaruhusu magari hayo barabarani.

" Kwa sasa tunadhama tunashirikiana na TBS, t unaweza kukagua system  ya gari, kwa hiyo utakapokamilisha gari hili, wataalamu wetu watafanya majukumu yao na kisha tutatoa ripoti tutakukabidhi,

"Ambapo ukieenda kwenye mamlaka yaani TBS wakiridhika utaipeleka ripoti hiyo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), lakini pia watahitaji ripoti ya ubora wa gari, tutashirikiana na NIT na anaamini baada ya hiyo ripoti kutoka magari hayo y atapata namba na kuingia barabarani," amesema Profesa Mganilwa

Hata hivyo, amesema kuwa wakati mabasi hayo hapo barabarani wataendelea kushirikiana kuona namna ambavyo wataweza kumsaidia Nyagawa kuendeleza ubora wa magari mengine ambayo yatakuwa kiwandani ili kuondoka mapungufu yaliyojitokeza katika basi la  kwanza kuundwa.

Mkuu huyo amesema, Serikali imewekeza vya kutosha katika chuo hicho ndiyo maana ameongozana na wataalam mbalimbali, wataalam wa mitambo ambao watamsaidia kutengeneza sehemu ya kuunganishia magari na jinsi biashara itakavyokuwa inaendelea wataendelea kujenga mitambo mingine.

Amesema ameongozana na wahandisi wa magari waliyobobea kupima ubora wa gari, kupima kiti cha dereva, viti vya abaria na pia kuangalia  uwiano wa mfumo wa gari kwa sababu basi hilo limeunganishwa na vifaa kutoka sehemu mbalimbali kama chases imetoka China.

"Nimekuja na wataalam wa fedha katika usafairishaji ambao wataweza kupiga hesabu za gharama zote, ambazo ukiongeza na faida, tutamshauri kutokana na ushindani wa soko uliyopo ili ajue litauzwa bei gani na pia wataalam wa masoko watamsaidia Nyagawa kutimiza ndoto zake,"amesema

Kwa upande wake, Nyagawa amesema alianza kazi hiyo mwaka 2012, ambapo ambapo Kampuni mama ya Budget Movers Ltd ilikopa Sh .bilioni sita, ambapo Sh.bilioni 2 zilitumika katika ujenzi wa kiwanda hicho na uunganishaji wa basi (BM Motors), kwa hiyo fedha hiyo ni ya mkopo wanaendelea kulipa utaratibu.

Amesema basi moja linaweza kuuzwa kwa zaidi ya sh milioni 200, lakini bado hawajapata bei ya uhakika kwa sababu bado  hayajakamilika na kulipiwa kodi  alisema mabasi hayo yalikuwa yakinunuliwa nje ya nchi zaidi ya Sh.milioni 300.

Pia, amesema hadi sasa bado hajapata jina la  basi hilo kwa hiyo anaomba wataalam wamsaidie kwa sababu ni gari la nchi.

Nyagawa amesema hadi basi hilo kufika hatua ya kukamilika wametumia kipindi cha mwaka mmoja na hiyo imechangia kwa sababu kuna baadhi ya vifaa (machine) vinakosekana.

Amesema alipotembelea chuoni hapo niliona wataalam wengi ambao watakuja kufanya kazi za kiinjinia, kwa sababu katika Kampuni yake hiyo hana wataalam wala mainjinia, mafundi wake wengi wanatoka VETA ambao na wao wanaujuzi wa magari, ambapo wengine alikuwa akisafiri nao nchi mbalimbali ili wazidi kujifunza.

Nyagawa amesema kuanzia sasa atachukua wataalam (Mainjinia) kutoka NIT maana yake ndiyo chuo cha Taifa, anaamini kitu kitakachofanyika hapo kitakuwa cha kitaifa.

" Kuna kipindi tukishindwa kuunda kitu fulani au kufunga nachukua wataalam kutoka China kuja kutusaidia kwa hiyo kwa sasa wataalam watatoka NIT, kwa tukisema tunataka kutengeza magari mawili kwa kila siku watahitaji wa zaidi ya 50 au watu 100, hao watu wote tunategemea kuwatoa NIT,"amesema Nyagawa

Akizungumza suala la kutaka Serikali imsaidie kitu gari, aliomba kuongezewa mtaji kwa sababu fedha zinazotakiwa kwenye kazi hizo ni nyingi na pia kupitia chuo hicho mambo mengi yatatatulika ikiwemo ya mashine za uundaji wa mabasi hayo.

Pia , ameshauri wafanyabiashara wawekeze kwenye viwanda ili uchumi wa Taifa uweze kukua kwa kasi ili kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na  Rais Dkt.John Magufuli ambayo inahamaishia uchumi wa viwanda.
 Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi, Profesa Zacharia Mganilwa akizungumza na waandishi wa baada ya tembelea Kiwanda cha kuunga magari kilichopo Kibaha Madafu mkoani Pwani. Kulia ni Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Kampuni ya BM Motors Ltd, Jonathan Nyagawa (Picha na Grace Gurisha)

Mafunzi wakiendela na kazi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...