BENKI ya NMB imekabidhi misaada mbalimbali ya vifaa tiba na vifaa vya elimu katika Mikoa ya Dar es Salaam na Kilimanjaro, ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa kurejesha kwa jamii asilimia moja ya faida yao kupitia Programu ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).

Jijini Dar es Salaam, NMB imetoa msaada yenye thamani ya Sh. Mil. 15 kwa Shule ya Sekondari Tambaza, iliyopo Upanga na Kituo cha Afya Pugu Kajiungeni wilayani Ilala jijini Dar es Salaam, wakati Mkoani Kilimanjaro imekabidhi vifaa tiba kwa Hospitali ya Wilaya ya Hai.

Tambaza Sekondari, imepokea msaada wa vitanda 80 vya kulalia wasichana wa shule hiyo vyenye thamani ya Sh. Mil. 10, vilivyokabidhiwa na Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd na kupokelewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Zungu.

Katika hafla ya kukabidhi vifaa tiba katika Kituo cha Afya Pugu Kajiungeni, NMB ilikabidhi msaada huo wenye thamani ya Sh. Mil. 5 kupitia kwa Meneja Mwandamizi wa NMB Kitengo cha Biashara za Serikali, Adelard Mangombo, na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala (DC), Sofia Mjema.

Mkoani Kilimanjaro, NMB kupitia Meneja wa Kanda ya Kaskazini, Aikansia Muro, alikabdhi msaada wa vitanda vitano vya kulalia, viwili vya kujifungulia akina mama, mashuka 25, magodoro 5, pamoja na hundi ya Sh. Milioni 16 kwa ajili ya wakulima wa zao la vanilla Mkoani humo.

 
Mkuu Wa Wilaya Mshikizi Agnes Hokororo (kushoto) akipokea sehemu ya msaada wa vifaa vinavyo tumika wakati akina mama wakijifungua kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini – Aikansia Muro.

NMB Karibu Yako
Meneja Mwandamizi wa NMB Kitengo cha Biashara za Serikali – Adelard Mang’ombo akimkabidhi msaada wa vifaa vya afya, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sofia Mjema ambavyo ni vitanda vitano pamoja na mashuka katika Kituo cha Afya Pungu Kajungeni vyote vyenye thamani ya shilingi milioni 5.
 Mkuu Wa Wilaya Mshikizi Agnes Hokororo (kushoto) akipokea sehemu ya msaada wa vifaa vinavyo tumika wakati akina mama wakifujingua kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini – Aikansia Muro.

NMB Karibu Yako

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...