Na Munir Shemweta, WANMM MUSOMA
Naibu Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amesema wizara yake itaipatia
ofisi ya ardhi mkoa wa Mara vifaa vya upimaji ili viweze kutumiwa na halmashauri
za mkoa huo kwa lengo la kuongeza kasi
ya upimaji.
Dkt Mabula alitoa kauli
hiyo jana wilayani Musoma mkoa wa Mara alipokwenda kukagua ofisi mpya ya ardhi
ya mkoa Mara ikiwa ni jitihada za wizara ya ardhi kusogeza huduma za ardhi kwa
wananchi.
Awali huduma za ardhi
zilikuwa zikitolewa na ofisi za Mkamishna Wasaidizi wa Kanda ambapo kanda moja
ilikuwa ikihudumia zaidi ya mikoa miwili jambo lililokuwa likiwapa usumbufu wamiliki
wa ardhi kwenda umbali mrefu kuifuata huduma hiyo.
Alisema, baada ya wizara
yake kuanzisha ofisi za mikao sasa wananchi watapata huduma za ardhi katika
mikoa husika na migogoro ya ardhi sasa itapatiwa ufumbuzi kupitia wataalamu
watakaokuwa katika mikoa hiyo.
Alibainisha kuwa, katika
jitihada za kuongeza kasi ya upimaji maeneo mbalimbali ofisi za mikoa zitapatiwa
vifaa vya upimaji ili visaidie halmashauri kupanga, kupima na kumilikisha ardhi
na kusisitiza vifaa hivyo vitatolewa bure na aliwataka wakurugenzi wa
halmashauri kushirikiana na ofisi za ardhi za mikoa.
Kwa mujibu wa Naibu
Waziri Mabula, Wizara yake imeamua kubeba jukumu la kutoa vifaa vya upimaji ili
kuongeza kasi ya upimaji ingawa jukumu hilio linapaswa kufanywa na halmashauri kwa
kuwa ndizo zenye mamlaka za upangaji miji katika maeneo.
Dkt Mabula
amesikitishwa na kiasi kidogo kinachotengwa na halmashauri kwa ajili ya kazi za
kupanga, kupima na kumilikisha ardhi ambapo alitolea mfano wa halmasahauri ya
Musoma kutenga milioni 30 kwa kazi mbalimbali za sekta ya kiasi alichokieleza
kuwa kidogo.
‘’Milioni 10 au 15 utapima
viwanja vingapi? Halmashauri hazijaipa kipaumbele sekta ya ardhi ndiyo maana
malalamiko yanakuwa mengi, muongeze bajeti za upimaji’’ alisema Dkt Mabula
Hata hivyo, ameishauri
halmashauri ya wilaya ya Musoma kuwatumia wataalamu wake kwa kuandika andiko ili
kupatiwa mkopo usio na riba unaotokewa na wizara kwa ajili ya shughuli za
umilikishaji ardhi ambapo alisema katika kipindi caha bajeti ijayo wizara
inatarajia kupata bilioni saba kwa ajili ya kuzikopesha almashauri.
Kwa upande wake Mkuu wa
wilaya ya Musoma Dkt Vincent Naano Anney aliipongeza wizara ya ardhi nyumba na
Maendeleo ya Makazi kwa uamuzi wake wa kuanzisha ofisi za mikoa na kueleza kuwa
uamuzi huo utaleta nafuu kwa wananchi wa
mara katika kupata huduma za ardjhi ambapo awali iliwalazimu kusagiri hadi Simuiyu
kupata huduma hiyo.
Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Mara Jerome
Kiwia akimuonesha Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt
Angeline Mabula sehemu ya Ofisi mpya za Ardhi mkoa wa Mara wakati Naibu Waziri
alipokwenda kuzikagua ofisi hizo mkoani Mara jana. Kulia kwa Naibu Waziri ni
Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dkt Vincent Naano Anney.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akikagua ofisi mpya za Ardhi mkoa wa
Mara wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi mkoani
Mara jana. Kulia kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dkt Vincent Naano
Anney na Kulia ni Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoa wa Mara Jerome Kiwia.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Dkt Angeline Mabula akioneshwa sehemu kitakachowekwa kibao cha
kuitambulisha ofisi mpya za Ardhi mkoa wa Mara na Kamishna Msaidizi wa Ardhi
Mkoa wa Mara Jerome Kiwia alipofanya ziara ya
kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi mkoani Mara jana (PICHA NA MUNIR SHEMWETA WIZARA YA ARDHI)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...