Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Ripoti ya Mwaka 2018-2019 kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Charles Kichere katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 26/03/2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akisoma Muhtasari wa Taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG ya Mwaka 2018-2019 iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Charles Kichere katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 26/03/2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia Makabrasha ya Taarifa Mbalimbali alizokabidhiwa na CAG katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Ripoti ya Mwaka 2018-2019 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo akisoma Muhtasari wa Taarifa yake ya Mwaka 2018-2019 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mara baada ya kutoka kwenye ukumbi wa Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma ambapo alipokea Ripoti mbili za Mwaka 2018/2019 kutoka Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa PCCB pamoja na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Makamu wa Rais Samia Suluhu, pamoja Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wakitoka kwenye ukumbi wa Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
PICHA NA IKULU
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...