Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ametembelea na kukagua Maendeleo ya Ujenzi wa Barabara ya Mabasi ya Mwendokasi Mbagala inayogharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 200 ambapo amemtaka Mkandarasi wa Mradi huo kuongeza kasi ili mradi ukamilike na kupunguza kero ya usafiri kwa wananchi wa Mbagala.

RC Makonda amesema kwa muda mrefu wakazi wa Mbagala walikuwa wakipata changamoto ya usafiri ikiwemo foleni na wakati mwingine wananchi kuibiwa simu na mikoba wakiwa wanagombania usafiri lakini kukamilika kwa mradi huo itakuwa mwarobaini wa kero zote zilizokuwa zikiwasumbua.

Aidha RC Makonda amesema kukamilika kwa barabara hiyo kutafanya Barabara ya Kilwa kuwa na Njia sita l, Madaraja Mawili Makubwa na Flyover jambo litakalosaidia kurahisisha shughuli za usafiri.

Aidha RC Makonda amezungumzia changamoto ya Mafuriko Mto Msimbazi kujaa eneo la Jangwani na kusababisha kusimama kwa shughuli za usafiri ambapo amesema Serikali ipo katika hatua ya kuanza kwa maboresho ya eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuinua Daraja na kufanya mto msimbazi kuwa sehemu ya utalii wa Boti ambapo ujenzi unatarajiwa kugharimu kiasi cha shulingi Bilioni 200.

Kuhusu Ugonjwa wa Corona, RC Makonda amesema tayari amewaelekeza Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanatenga maeneo maalumu ya kuwahifadhi watu wote wanaotoka nje ya Nchi (karantini) ili wakae chini ya uangalizi kwa muda wa siku 14 huku akiwahimiza wananchi kuendelea kuchukuwa tahadhari dhidi ya Virusi hivyo vya Corona.

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Paul Makonda (kuliia) akikagua maendeleo ya mrad Ujenzi wa Barabara ya Mabasi ya Mwendokasi Mbagala wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam,inayogharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 200 leo Machi 23, 2020 ambapo amemtaka Mkandarasi wa Mradi huo kuongeza kasi ili mradi ukamilike na kupunguza kero ya usafiri kwa wananchi wa Mbagala.(Picha  zote na Emmanuel Massaka,Michuzi Tv)

Mafundi wakiendi kazi ya ujenzi wa Barabara ya Mabasi ya Mwendokasi Mbagala wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam leo Machi 23, 2020.


 Muonekano wa Barabara ya Mabasi ya Mwendokasi Mbagala wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.(Picha zote, Emmanuel Massaka,Michuzi Tv)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...