NA TIGANYA VINCENT
MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na
kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilaya ya Sikonge kumkamata Mganga
Mfawidhi wa Zahanati ya Tutuo Longa Magasha na kuchunguza tuhuma za
malipo ya fedha ya milioni moja kwa kazi hewa ya ukarabati wa kisima.
Alisema kiasi hicho cha fedha zilitolewa kupitia fedha ambazo Zahanati
hiyo ilipata kutokana na Malipo kwa Ufanisi (RBF) kwa lengo kufanyia
ukarabati wa kisima lakini haionyeshia kama kuna kazi imefanyika.
Mwanri ametoa kauli hiyo jana wakati wa ziara ya ukaguzi wa
utekelezaji wa shughuli za Malipo kwa Ufanisi (RBF) kwenye Vituo na
Zahanati mbali katika Wilaya ya Sikonge.
Alisema baada ya kumhoji Mhasibu wa Zahanati hiyo alimweleza kuwa
Mganga huyo kupitia Dokezo alimtaka amlipe yeye kiasi cha fedha hizo
ili akawalipe mafundi na vibarua walioshiriki kazi ambayo haionekani.
Mwanri alisema Mganga huyo asimame kupisha uchunguzi wa TAKUKURU kama
itaonyesha kumefanyika wizi wa fedha za umma apelekwe Mahakamani na
kama itaonyesha hakuna kosa basi aendelee na kazi yake.
Akizungumza katika mkutano huo Mkuu wa TAKUKURU wilayani Sikonge
Magore Msena alisema walishapata taarifa za matumizi mabaya fedha za
umma katika mradi huo wa kisima na walikuwa wakiendelea na uchunguzi
na walikuwa mbio kuwachukulia hatua wahusika.
Alisema uchunguzi wa awali walibaini kuwa ni kiasi cha shilingi
milioni mbili na sio milioni moja ndio kinaonekana kutumika katika
kazi hiyo hewa .
Mkuu wa Mkoa wa Tabora akiwa wilayani Sikonge amefanikiwa kukagua
Kituo cha Afya Mazinge, Zahanati ya Tutuo, Zahanati ya Pangale na
Zahanati ya Usesula.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akizungumza jana na wagonjwa
katika Zahanati ya Tutuo wilayani Sikonge wakati wa ziara ya ukaguzi
wa utekelezaji wa shughuli za Malipo kwa Ufanisi (RBF) kwenye Vituo na
Zahanati mbali katika Wilayani humo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...