Rwanda imethibitisha kisa chake cha kwanza cha virusi vya Corona (COVID-19). Mgonjwa huyo ni raia wa India aliyewasili Rwanda Machi 8 kutoka Mumbai, India, kulingana na taarifa iliyotolewa na wizara ya afya.

Raia huyo hakuwa na dalili zozote za virusi vya Corona wakati anawasili nchini Rwanda na alijipeleka mwenyewe kwenye kituo cha afya Machi 13, ambapo alifanyiwa vipimo mara moja.

Wizara ya afya imesema kwa sasa anaendelea na matibabu, hali yake imeimarika na ametengwa na wagonjwa wengine.

Wote aliotangamana na mgonjwa huyo wanaendelea kutafutwa katika juhudi za kuudhibiti ugonjwa huo.

''Raia wote wa Rwanda wanastahili kufuata sheria zote zilizotolewa na wizara ya afya hasa kuhusu kuosha mikono kila mara,'' taarifa hiyo imesema.
 
Pia imesihi raia kutohudhuria mikusanyko ya umma na kuarifu mamlaka iwapo watashuhudia tukio wanalolishuku kupiga simu kupitia nambari 114.

Kupitia mahojiano na kituo cha redio cha taifa cha Radio Rwanda, Dr Ngamije Daniel, Waziri wa Afya wa Rwanda amesema kwamba nchi yake iko tayari kupambana na virusi hivyo.

''Nchi iko tayari ... kwa misingi wafanyakazi wenye ujuzi...''

Waziri Dr Ngamije pia amesema kwamba katika kipindi cha wiki mbili zijazo kuanzia Jumamosi, mikusanyiko ambayo sio lazima au makutano yoyote ya watu imepigwa marufuku. 
 Dr Ngamije Daniel, Waziri wa Afya Rwanda, amesema nchi iko tayari kukabiliana na Corona.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...