Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii
SERIKALI imetoa wito kwa wananchi kuacha kutoa rushwa kwa wahudumu wa afya pindi wanapopatiwa huduma kwani kutoa kutoa huduma ni wajibu wao.
Hayo ameyasema Mkurugenzi wa Huduma za Kinga wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Wanawake Wanataka Nini inayoratibiwa na Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama Tanzania ikiwa ni maadhimisho ya Utepe Mweupe Tanzania ambayo hufanyika Kila Machi 15 ya kila mwaka.
Maadhimisho hayo ni kuwakumbuka akina mama ulimwe guni waliopoteza maisha wakati wa kujifungua kutokana na sababu mbalimbali.
Dkt. Subi amesema utafiti mdogo uliofanywa unaonesha vifo vitokanavyo na uzazi vimepungua kutoka 1744 mwaka 2018 hadi kufikia 1657 kwa mwaka 2029
Dkt. Subi alimwakilisha Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema kuwa serikali inaendelea kuboresha huduma za afya ili kila mtu apate huduma huduma bora hivyo mwananchi kupata huduma ni haki yake.
"Katika kipindi cha miaka minne serikali imeweza kujenga Hospitali 70 ambapo miaka zaidi ya 50 ya uhuru kulikuwa na hospitali 77 tu katika kila Mkoa mpya tumejenga hospitali na vituo vya afya 540 vimejengwa na vingine kukarabatiwa.
"Tumeboresha Miundombinu ya vituo vya afya 361 lengo letu ni kuwasikiliza wanawake wanakochotaka hivyo idadi ya akinamama wanaojifungulia vituo vya afya imeongezeka mwanzo ilikuwa asilimia 63 lakini sasa wamefikia asilimia 79,"alibainisha Dk Subi.
Aidha amesema upatikanaji wa dawa umeongezeka ambapo kwasasa dawa muhimu zinapatikana kwa asilimia 94 huku chanjo zinapatikana kwa asilimia 98.
"Ongezeko hilo la dawa limetokea baada ya bajeti ya dawa kuongezwa kutoka Sh bilioni 30 hadi Sh bilioni 270.
Dkt. Subi amesema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Taasisi ya Taifa ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)na taasisi zingine za serikali na zisizo za kiserikali wanatarajia kukamilisha utafiti wa vifo vitokanavyo na uzazi.
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga aliwataka wanaume kuwasikiliza wake zao nini wanachotaka hasa kipindi cha ujauzito ili kuwapunguzia mawazo.
Kwa upande wake Mratibu wa Utepe Mweupe nchini Rose Mlay aliiomba serikali kuongeza idadi ya wauguzi katika vituo vya afya ili kinamama wapate huduma nzuri.
"Tunaomba wizara ya afya iongeze wakunga wa kutoka katika kila kituo cha afya angalau wawe wakunga watano wanaofanya kazi ya ukunga tu kwani kwa sasa ukienda utakuta mkunga mmoja au wawili.
"Kwa hospitali za Wilaya wawe 20 na kwa hospitali ya Rufaa na Mkoa wawe 102 wanaofanya kazi za ukunga tu,"alieleza Mlay.
Alisema utafiti walioufanya katika Mikoa 10 kwa kuwauliza wanawake 110,000 alisilimia ya wanawake 8.61 walitaka huduma za uzazi zenye heshima na utu.
"Asilimia 8.99 walitaka madawa na vifaa ,asilimia 7.56 walitaka huduma zilizoboreshwa ba ustawi na afya ya uzazi kwa ujumla,asilimia 7.32 walitaka kuongezwa vituo vya afya vyenye ukamilifu na waliotaka ushauri nasaha na ufahamu kuhusua afya ya uzazi walikuwa 7.17,"alisema Mlay.
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia, Wazee na Watoto wakiwa na chapisho lililozinduliwa pamoja na washirika wa Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama Tanzania.
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Leonard Subi akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Wanawake Wanataka Nini inayoratibiwa na Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama.
Mratibu wa Utepe Mweupe Rose Mlay akitoa maelezo kuhusiana na Uzinduzi wa Kampeni ya Wanawake Wanataka Nini katika kupatiwa huduma za uzazi iliyozinduliwa katika maadhimisho ya Siku ya Ute
Mashauri Mwandamizi wa Afya ya Mama na Mtoto wa Jhpiego Jasmine Chadewa akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi wakati akipita katika maonesho ya Siku ya Utepe Mweupe jijii Dar es Salaam.
Khadija Rajab akitoa ushuda namna alivyopata huduma na kusababisha madhara wakati kujifungua katika maadhimisho ya Siku ya Utepe Mweupe jijini Dar es Salaam.
Ashura Juma akitoa ushuhuda wa namna alivyopata huduama kwa kukutana na changamoto ya watoa huduma wasio na weledi.
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Leonard Subi akikata Utepe kuashiria Uzinduzi wa Kampeni ya Wanawake Wanataka Nini katika maadhimisho siku ya a Utepe Mweupe yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi Dkt. Leonard Subi akiwa Katia picha ya pamoja na Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...